Kilomita 33 za Lami kuwanufaisha wananchi Iringa kupitia mradi wa Rise

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika barabara ya Wenda-Mgama Km 19...

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika barabara ya Wenda-Mgama Km 19 na Mtili-Ifwagi Km 14 katika Wilaya ya Iringa na Mufindi mkoani Iringa.

Barabara hizo zinazojengwa chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) zinalenga kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Akiongea katika mahojiano maalum, Meneja wa TARURA Wilaya ya Mufindi, Mhandisi Richard Sanga amesema kuwa ujenzi wa barabara hizo unalenga kuwezesha wananchi katika shughuli za kilimo na biashara.

“Kukamilika kwa barabara hii ya Mtili – ifwagi kutaiwezesha Wilaya ya Mufindi kufikisha barabara za lami zenye urefu wa Kilomita 87.3 na kuendelea kukuza uchumi wa wananchi”, amesema Mhandisi Sanga.

Naye, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa RISE, Mhandisi Joel Mwandobo amesema ujenzi wa barabara hizo unategemea kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2025 na amemtaka Mkandarasi kampuni ya CHICO kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa.

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inatekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) katika Mikoa ya Iringa, Geita, Tanga na Lindi ili kuendelea kuboresha uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

The post Kilomita 33 za Lami kuwanufaisha wananchi Iringa kupitia mradi wa Rise first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/4nVro9w

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kilomita 33 za Lami kuwanufaisha wananchi Iringa kupitia mradi wa Rise
Kilomita 33 za Lami kuwanufaisha wananchi Iringa kupitia mradi wa Rise
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/11/IMG_9213-950x711.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/kilomita-33-za-lami-kuwanufaisha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/kilomita-33-za-lami-kuwanufaisha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy