Mamlaka za biashara waleeni wajasiriamali sio kuwafungia biashara.
HomeHabariTop Stories

Mamlaka za biashara waleeni wajasiriamali sio kuwafungia biashara.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameagiza Mamlaka za udhibiti na usimamizi wa biashara nchini kuachana na dhana ya kukimbili...

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameagiza Mamlaka za udhibiti na usimamizi wa biashara nchini kuachana na dhana ya kukimbilia kufunga na kukwamisha wajasiriamali wadogo ambao hawajatimiza vigezo vya kisheria badala yake wawe walezi kwa kuwaelekeza hatua za kufuata ili wawe walipa kodi wakubwa.

Kigahe ametoa Maelekezo hayo mapema leo wakati akifungua maonesho ya tatu ya Biashara ya ‘Tanzanite Manyara Trade Fair 2024’ Mjini Babati, Manyara yanayohudhuriwa na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya Tanzania.

“Niziagize Mamlaka zinazosimamia na kudhibiti biashara kuwalea na kuwapa miongozo sahihi wajasiliamali badala ya kuwafungia pindi wanapokosea ili kuendeleza kukuza uchumi wa nchi yetu,” amesema Naibu Waziri Kigahe.

Kwa Upande wake Meneja Biashara Mati SuperBrand Gwandumi Mpoma ambao ni wadhamini wakuu, amewaomba wajasiliamali kuendelea kujitokeza kushiriki maonesho hayo ili kuweza kutangaza bidhaa zao zaidi.

Ametoa rai kwa Makampuni mengine makubwa kujitokeza kudhamini maonesho hayo ili kuisaidia serikali ili kuwasaidia wajasiliamali na wafanyabiashara ambapo huu ni mwaka wa tatu mfululizo tokea waanze kudhamini.

Ameongeza kuwa mwamko wa wafanyabishara wa mkoa wa Babati wamekosa mwamko wa kushiriki na kuzidiwa na wageni ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kutoka nchi mbali mbali kama vile Uganda, Kenya.

Nae Katibu mtendaji Chama cha Wafanyabiashara- TCCIA mkoa wa Manyara Zainabu Rajabu amesema maonesho ya mwaka huu yamehudhuriwa na washiriki 337 chini ya kauli mbiu ya “Manyara kwa ustawi wa biashara na uwekezaji” huku baadhi ya wajasiriamali walioshiriki wakifurahia kukutanishwa na wateja ma marafiki wa kibiashara.

Maonesho ya tatu ya Biashara ya Tanzanite Manyara trade fair 2024 yaliyoanza Oktoba 20 yataendelea hadi Oktoba 30.

The post Mamlaka za biashara waleeni wajasiriamali sio kuwafungia biashara. first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/dFSAPhz
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mamlaka za biashara waleeni wajasiriamali sio kuwafungia biashara.
Mamlaka za biashara waleeni wajasiriamali sio kuwafungia biashara.
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/10/IMG-20241024-WA0003-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/mamlaka-za-biashara-waleeni.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/mamlaka-za-biashara-waleeni.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy