Serikali yaanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari
HomeHabariTop Stories

Serikali yaanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari

Serikali kupitia wizara mbili zenye dhamana ya mawasiliano na uchikuzi Tanzania bara na Zanzibar zimeanzisha mchakato wa kuridhia mikataba y...

Serikali kupitia wizara mbili zenye dhamana ya mawasiliano na uchikuzi Tanzania bara na Zanzibar zimeanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari kwa kusimamia ulinzi wa sekta hiyo pamoja na kuendesha vyombo kwa usalama.

Uharibifu wa mazingira katika upande mmoja wa dunia unaweza kuleta athari kubwa sehemu mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na nchini kwetu, hali inayopelekea kuanzishwa kwa Mikataba ya Kimataifa inayohusu masuala mbalimbali ya hifadhi ya mazingira, kwa lengo la kuweka juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto hizo na kuendelea kuhifadhi mazingira kwa pamoja kama urithi wa dunia kwa vijavyo.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji na miaka 50 ya IMO hii leo Septemba 23 katika viwanja vya Mkendo ,manispaa ya Musoma mkoani Mtwara Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA) Bi. Mtumwa Said Sandal amesema kuwa na uwepo wa elimu ya kutosha juu ya utunzaji wa mazingira itasaidia wananchi kuwa na uelewa zaidi juu ya utunzaji na udhibiti wa usalama mazingira.

‘Siku ya Bahari Duniani ni kuelimisha umma kuhusu jinsi wanadamu wanavyoathiri bahari, kuendeleza harakati za kimataifa zinazotetea bahari zetu, na kuhamasisha na kuunganisha watu duniani kote kuchukua hatua ya kuwaokoa’.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi – Zanzibar, Bw. Makame Haji ametoa rai kwa Watanzania kutunza mazingira ya usafirishaji majini ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba Maalum wa Kimataifa wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) unaozuia uchafuzi wa mazingira majini unaotokana na shughuli zinazofanyika katika Meli (MARPOL) wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Usafiri kwa njia ya Maji,  tarehe 23 Septemba, 2024 katika viwanja vya Mkendo vilivyopo katika Wilaya ya Musoma, mkoani Mara.

“Serikali tayari imesharidhia mkataba huu pamoja na kanuni zake (Annex) tano kati ya sita ilizotolewa na IMO na tumeshaanza kutekeleza mikakati yake. Kwa sasa tunajenga Kituo kikuu cha Ufuatiliaji na Uokoaji (MRCC) kwa ajili ya Ziwa Victoria ambacho kitatumika kupitia ukanda Afrika Mashariki huku akiweka bayana umuhimu wa Sekta ya Uchukuzi,” ameongeza Bw. Haji.

Maadhimisho ya Siku ya Usafiri kwa Njia ya Maji yamefunguliwa rasmi leo na Mhe. Makame Machano Haji kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed na kilele chake kitakuwa tarehe 26 Septemba 2024.

 

The post Serikali yaanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/P7GEckd
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali yaanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari
Serikali yaanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/09/04a19736-4476-4141-90c8-c3d0583127aa-950x760.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/serikali-yaanzisha-mchakato-wa-kuridhia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/serikali-yaanzisha-mchakato-wa-kuridhia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy