Waziri Makamba awaasa Marekani kuliishi Azimio la Uhuru
HomeHabariTop Stories

Waziri Makamba awaasa Marekani kuliishi Azimio la Uhuru

Katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 248 ya Uhuru wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January M...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 10, 2024
WHO yafanya uchunguzi wa mlipuko mpya wa ugonjwa usiojulikana Kongo
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 9, 2024

Katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 248 ya Uhuru wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), ameishukuru na kuipongeza Marekani kwa mchango wake katika maendeleo ya Tanzania huku akiwasihi kukumbuka na kuenzi yale waliyoazimia Julai 4, 1776.

Waziri Makamba amezungumza hayo akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika makazi ya Balozi Michael Battle jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Makamba alikuwa mgeni rasmi.

Amewataka Marekani kuwa mstari wa mbele na mfano wa uongozi bora duniani na wenye kulinda amani na kuunganisha watu ili kuiishi taswira ya Dunia yenye haki, isiyo na upendeleo, yenye kujali na isiyo na ubaguzi kama inavyotajwa kwenye Azimio la Uhuru wa Marekani. “Tunatumai, tunatarajia na tunajua kwamba inawezekana kwa nchi hii kubwa ulimwenguni itaendelea kuwa thabiti katika utumiaji wake wa maadili ambayo yanashikilia ubinadamu pamoja,” ameongeza Waziri Makamba.

Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza kuwa hakuna nchi inayojitosheleza binafsi na kuwa changamoto za duniani kote kwa sasa zinahitaji ushirikiano na umoja wa kimataifa ili kutatuliwa, huku akipongeza mabalozi kwa kazi nzuri wanazofanya kuziunga nchi zetu

Tanzania na Marekani zimekuwa na ushirikiano wa uwili kwa miaka 63 huku kwa pamoja zikitazamia kuendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zote mbili kwa manufaa ya wananchi wake.

.
.
.
.
.
.

The post Waziri Makamba awaasa Marekani kuliishi Azimio la Uhuru first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/m9wbk7G
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Makamba awaasa Marekani kuliishi Azimio la Uhuru
Waziri Makamba awaasa Marekani kuliishi Azimio la Uhuru
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/07/Snapinsta.app_449762438_18076360171502573_1047340370733188115_n_1080-950x669.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/waziri-makamba-awaasa-marekani-kuliishi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/waziri-makamba-awaasa-marekani-kuliishi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy