Viongozi wa Dini Kagera wamuombea Rais Samia, Bashungwa awasilisha mchango harambee
HomeHabariTop Stories

Viongozi wa Dini Kagera wamuombea Rais Samia, Bashungwa awasilisha mchango harambee

Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kagera wameungana kwa pamoja kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Has...

Rais Samia aipongeza REA
Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 5, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 5, 2024

Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kagera wameungana kwa pamoja kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa Kitaifa na Serikali kwa kuendelea kudumisha Amani, Utulivu, Upendano na Maelewano.

Ibada hiyo iliyowakutanisha viongozi wa Dini ya Kikristo na Kiislamu imefanyika leo Julai 28, 2024 katika Kanisa Anglikana Mt. Yohana Kimbugu – Muleba, Kagera iliyoambatana na Ibada ya Shukrani ya Miaka 12 ya Uchungaji wa Askofu Grayson Mutegeki Katunzi pamoja na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa.

Akiongoza Ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Lweru Kanisa la Anglikana Tanzania, Godfrey Mbelwa amesema viongozi wa Dini na Waumini wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa Kitaifa kwani wanafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi Maendeleo.

“Tunawaombea Viongozi wetu kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bunge, Mahakama, Jeshi, Ulinzi na Usalama na wote wenye mamlaka mbalimbali katika nchi hii”- amesema Askofu Godfrey katika maombi yake.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru viongozi wa Dini kwa kuandaa maombi ya kumuombea Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyoambatana na Harambee ya Ujenzi ya wa Kanisa Parishi ya Kimbugu, Muleba mkoani Kagera.

“Serikali ya Awamu ya sita inaendelea kujenga mshikamano, umoja kwa kushirikiana na viongozi wa dini ili kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa hofu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumtii”, amesisitiza Bashungwa.

Katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa, Waziri Bashungwa amewasilisha mchango wa Viongozi wa Serikali, jumla ya Shilingi Milioni 30 na kuahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Kanisa hilo ili ujenzi ukamilike kwa wakati.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuwasihi waumini kuwa wacha Mungu ili kuwa na hofu ya kutenda maovu kwenye jamii ikiwemo mauaji na ukatili wa kijinsia.

.
.
.
.

 

The post Viongozi wa Dini Kagera wamuombea Rais Samia, Bashungwa awasilisha mchango harambee first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/4rpXswJ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Viongozi wa Dini Kagera wamuombea Rais Samia, Bashungwa awasilisha mchango harambee
Viongozi wa Dini Kagera wamuombea Rais Samia, Bashungwa awasilisha mchango harambee
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/07/WhatsApp-Image-2024-07-28-at-6.46.14-PM-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/viongozi-wa-dini-kagera-wamuombea-rais.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/viongozi-wa-dini-kagera-wamuombea-rais.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy