TUME ya Ushindani FCC yawahakikishia wawekezaji mazingira salama ya kuwekeza nchini
HomeHabariTop Stories

TUME ya Ushindani FCC yawahakikishia wawekezaji mazingira salama ya kuwekeza nchini

TUME ya Ushindani (FCC) imewahakikishia wawekezaji kutoka nje ya nchi wanaokuja nchini Tanzania kuwekeza kwani kuna mazingira salama ya uwek...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 24, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 24, 2024
Alikiba akishirikia na Asas waandaa tamasha la ASAS FIT & FUN KIDS FEST

TUME ya Ushindani (FCC) imewahakikishia wawekezaji kutoka nje ya nchi wanaokuja nchini Tanzania kuwekeza kwani kuna mazingira salama ya uwekezaji pamoja na kufanyabiashara.

 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Kudhibiti bidhaa bandia duniani ambayo huadhimishwa kati ya Juni na Julai ya kila.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikihimiza wawekezaji kutoka nje kuja nchini ili kufanya uwekezaji pamoja na biashara sambamba na kudhibiti ubora.

 

Kuhusu ubora wa bidhaa ,Erio amewashauri wananchi kuacha mara moja matumizi ya bidhaa bandia na badala yake wanunue na kutumia bidhaa halisi ili kusaidia kuchochea uwekezaji, kukuza fursa za ajira na hatimaye kuchagiza ukuaji wa uchumi wao na taifa kwa ujumla.

“Tusikubali kununua bidhaa bandia na hii itasaidia hata wale wanaokuja kuwekeza watakapofanya tathimini ya bidhaa zilizopo wakute tunatumia bidhaa halisi na zilizobora.”

 

Pia amesema kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara zinayofanyika ulimwenguni zinahusisha bidhaa bandia huku akibainisha baadhi ya madhara ya bidhaa hizo kuwa ni kutopata thamani halisi ya fedha pamoja na madhara mbalimbali ya kiafya kwa watumiaji

Akizungumzia Wiki ya kudhibiti bidhaa bandia duniani amesema wiki hiyo inaadhimishwa sehemu zote duniani kati ya Juni na Julai na sababu yake ni kwamba bidhaa bandia zina changamoto nyingi.

Ametaja baadhi ya athari za bidhaa bandia kuzorotesha biashara, uchumi na kukosena kwa ajira nchini.”Bidhaa bandia zina matatizo hata katika maeneo ya kiuchumi kwanza zinaathiri ubunifu kwasababu katika kushindana unatakiwa kila kitu uje na kitu kipya kuwa na bidhaa katika uchumi kunadhorotesha biashara.

 

Katika maadhimisho ya mwaka huu kauli mbiu inasema Kudumisha uhalisia kwa kulinda ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi nchini na inatarajiwa kuadhimishwa Julai 18 katika ukumbi wa mikutano ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Pia katika maadhimisho hayo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya wajasiriamali na wamiliki wa viwanda vidogovidogo pamoja na majadiliano ya jopo.

The post TUME ya Ushindani FCC yawahakikishia wawekezaji mazingira salama ya kuwekeza nchini first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/9yjNvkT
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: TUME ya Ushindani FCC yawahakikishia wawekezaji mazingira salama ya kuwekeza nchini
TUME ya Ushindani FCC yawahakikishia wawekezaji mazingira salama ya kuwekeza nchini
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/07/IMG-20240717-WA0170.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/tume-ya-ushindani-fcc-yawahakikishia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/tume-ya-ushindani-fcc-yawahakikishia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy