Naibu Waziri Chande aipa kongole benki ya Mkombozi.
HomeHabariTop Stories

Naibu Waziri Chande aipa kongole benki ya Mkombozi.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameipongeza Benki ya Biashara ya Mkombozi,kuwa imepanda kutoka hatua moja kwenda nyingine ndani ya muda ...

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameipongeza Benki ya Biashara ya Mkombozi,kuwa imepanda kutoka hatua moja kwenda nyingine ndani ya muda mfupi huku amewasihi watendaji wa Benki hiyo kutoridhika na hatua waliyofikia, badala yake waendelee kufanya uhamasishaji ili kuifanya Mkombozi Benki iendelee kukua.

Akizungumza Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande katika Hafla ya Mkombozi Benki kupandishwa Rasmi kutoka Soko la Ukuzaji Mitaji la DSE (EGM) na kwenda kwenye Soko Kuu la Uwekezaji (MIMS) iliyofanyika Kambarage House jijini Dar es Salaam.

“Hongereni sana Mkombozi Bank kwa hatua hii mliyofikia, kwa sababu mmepanda hadhi kutoka hatua moja kwenda nyingine ndani ya muda mfupi sana. Lakini niwaombe, msiridhike na hatua hiyo mliyoifikia, kwa sababu kuna maneno yanasema ‘Mpanda patosha, huvuna pa mkwisha.”

“Endeleeni kuhamasisha ili Bank hii ya Mkombozi iendelee kukua. Kwa hiyo naomba kutangaza rasmi kwamba Mkombozi Bank imepandishwa rasmi kutoka Soko la Ujasiriamali (EGM) na kuingizwa Katika Soko Kuu la Uwekezaji (MIMs),” amesema Naibu Waziri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Respige Kimati amesema kuwa Benki hiyo imewekeza nguvu nyingi ili kuanza kutoa gawio kwanzia mwakani 2025, kuwa Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuungana na Serikali katika kuwashika mkono watu waliopatwa na majanga mbalimbali ndani ya jamii.

“Tumeshuhudia ukuaji mkubwa wa faida, ongezeko la amana za wateja, ongezeko la mikopo iliyotolewa kwa watanzania hasa sekta binafsi, kupanuka kwa mtandao wetu wa matawi na uwekezaji mzuri katika huduma za benki kwa njia ya Mtandao, hususani uanzishwaji na usambazaji wa huduma za Benki kwa njia wa Mawakala”. amesema Kimati

Aidha, Kimati amesema Malengo ya benki hiyo ni kumkomboa Mtanzania katika wimbi la umasikini kwa kutoa huduma za kibenki hasa mikopo midogo midogo kwa watu binafsi wakiwemo vijana na wanawake na mikopo ya kati na mikubwa kwa makampuni, taasisi za huduma na wafanyabiashara wa kati na wadogo.

Hivyo, hatua hii mpya ya kuwa sehemu ya Soko Kuu la Uwekezaji (MIMS) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, tunayo imani kubwa kwamba mafanikio zaidi yanakuja mbele yetu, tunahitaji kuendelea kupata msaada wenu wa dhati na tunawaomba washirika wetu, wateja wetu, wanahisa, mamlaka mbalimbali za usimamizi wa sekta ya fedha nchini na watunga sera kuendelea kutuunga mkono katika safari hii ili Msaada wenu ni muhimu sana katika kuhakikisha tunatimiza malengo yetu ya muda mrefu na kuboresha huduma zetu kwa wateja wetu.

The post Naibu Waziri Chande aipa kongole benki ya Mkombozi. first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/ONvKaYR
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Naibu Waziri Chande aipa kongole benki ya Mkombozi.
Naibu Waziri Chande aipa kongole benki ya Mkombozi.
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/06/IMG-20240614-WA0034.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/06/naibu-waziri-chande-aipa-kongole-benki.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/06/naibu-waziri-chande-aipa-kongole-benki.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy