Tanzania yasisitiza ushirikiano kukabiliana na malaria
HomeHabari

Tanzania yasisitiza ushirikiano kukabiliana na malaria

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inaendelea kuongeza jitihada mbalimbali katika kukabili ana na ugonjwa wa Malaria pamo...


Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inaendelea kuongeza jitihada mbalimbali katika kukabili ana na ugonjwa wa Malaria pamoja na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika (NTDs).

Makamu wa Rais amesema hayo huko Kigali Rwanda wakati wa mkutano uliolenga kuunganisha nguvu za pamoja katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria pamoja na magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.

Ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano wa wadau ili kufanya uwekezaji katika upatikanaji wa kinga, upimaji wa magonjwa, matibabu, ufuatiliaji wa magonjwa pamoja na kuunganisha uvumbuzi na tafiti ili kuharakisha kufikia malengo na ahadi za mwaka 2018 ambazo zililenga kuondoa malaria katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ifikapo mwaka 2023.

Pia Dkt. Mpango amesema Tanzania kwa sasa inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano wa programu ya kudhibiti magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele (2021 – 2026) unaolenga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kudhibiti na kutokomeza magonjwa hayo.

Amesema tayari mafanikio mbalimbali yamepatika nchini Tanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa malaria ikiwemo kufikia chini ya asilimia moja kuenea kwa ugonjwa huo Zanzibar pamoja na mikoa mitano ya Tanzania bara ambapo lengo katika maeneo hayo ni kuondoa kabisa ugonjwa huo ifikapo mwaka 2025.

Makamu wa Rais yupo nchini Rwanda kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa 26 wa wakuu wa serikali wa nchi wanachama za Jumuiya ya Madola.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania yasisitiza ushirikiano kukabiliana na malaria
Tanzania yasisitiza ushirikiano kukabiliana na malaria
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6_uXeV6NartFc_ySpOzCc7CT38i3LpPcosfAfEljZOk61kIhShPQa62dKFjjLGKrtMvhVLtt54gPExEs8Ru2h35psU92VH4Et55oK_yN6GEn9rptVNvOTszrTnq9dGUEGzd01jcAUZIogr1dZXCPZxSez-P6kUvc3EZV_aIs4tWeNDNh7VkeBprX2lA/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6_uXeV6NartFc_ySpOzCc7CT38i3LpPcosfAfEljZOk61kIhShPQa62dKFjjLGKrtMvhVLtt54gPExEs8Ru2h35psU92VH4Et55oK_yN6GEn9rptVNvOTszrTnq9dGUEGzd01jcAUZIogr1dZXCPZxSez-P6kUvc3EZV_aIs4tWeNDNh7VkeBprX2lA/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/tanzania-yasisitiza-ushirikiano.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/tanzania-yasisitiza-ushirikiano.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy