Makamu Wa Rais Apokea Gawio La Serikali Kutoka Nmb June 15

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameagiza Mashirika ambayo Serikali ina hisa kuhakikisha y...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameagiza Mashirika ambayo Serikali ina hisa kuhakikisha yanaanza kutoa Gawio kwa serikali mara moja, pia Taasisi zinazotakiwa kutoa asilimia 15 ya mapato ghafi kwa mujibu wa sheria zifanye hivyo kikamilifu na kwa wakati.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa hafla ya kupokea Gawio la shilingi bilioni 30.7 kutoka kwa Benki ya NMB iliofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2022. Amesema Mashirika ambayo yanategemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Serikali yanapaswa kuwa na  mikakati madhubuti na inayotekelezeka ya kupunguza utegemezi kwa Serikali na kumuagiza  msajili wa Hazina kuhakikisha  wakuu wa taasisi husika wanatekeleza maagizo hayo.

Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha na kuweka mazingira rafiki na endelevu ya kufanya biashara katika sekta ya fedha na sekta zote nchini. Pia ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii nchini (corporate social responsibility) sambamba na kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato. Amewaasa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kuboresha  huduma za kijamii kwenye sekta mbalimbali kama afya,elimu na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na  kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na tabiawatu.

Kwa Upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Wizara itaendelea kusimamia maelekezo ya kuhakikisha taasisi za serikali na zile ambazo serikali ina hisa zinatoa Gawio. Aidha amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za sekta binafsi ili kuweza kuhakikisha zinafanya kazi vizuri.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema Gawio la Serikali kutoka Benki ya NMB limeendelea kukua kila mwaka na kuwa endelevu mpaka kufikia bilioni 30.7 kwa mwaka 2022 kutoka bilioni 10.48 mwaka 2018. Amesema adhma ya NMB ni kuleta tija kwa wawekezaji ikiwemo serikali ambayo inamiliki hisa za asilimia 31.8.

Aidha Bi Zaipuna ameongeza kwamba Benki ya NMB itaendelea kuwa mdau mkubwa wa serikali katika kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa kupitia uwekezaji katika sekta ya kilimo na biashara. Amesema mpaka mwezi Desemba 2021 jumla ya mikopo ya shilingi Trilioni 4.3 imetolewa kwa wakulima na wafanyabiashara.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Makamu Wa Rais Apokea Gawio La Serikali Kutoka Nmb June 15
Makamu Wa Rais Apokea Gawio La Serikali Kutoka Nmb June 15
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJ5rArSWYp-MRo4zAc1603LNA4HcTlzA4gW5-aM1E2Es1HWJUwCtTFlRxpyKsXL7TwoXXzxPjbwE7NNYMNsJokhNCCX_r2RzbQocelGZh0tldxQ0oADLy1-nMsx0vhzuUQox5s78aAV-YT49iGuTWpzYp2b_q_ZQmK3cXRzKFlk8E7ZpME8ZItAbxYAQ/s16000/00003-1536x997.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJ5rArSWYp-MRo4zAc1603LNA4HcTlzA4gW5-aM1E2Es1HWJUwCtTFlRxpyKsXL7TwoXXzxPjbwE7NNYMNsJokhNCCX_r2RzbQocelGZh0tldxQ0oADLy1-nMsx0vhzuUQox5s78aAV-YT49iGuTWpzYp2b_q_ZQmK3cXRzKFlk8E7ZpME8ZItAbxYAQ/s72-c/00003-1536x997.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/makamu-wa-rais-apokea-gawio-la-serikali.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/makamu-wa-rais-apokea-gawio-la-serikali.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy