Shirika la Afya Duniani, WHO, haliamini kwamba mlipuko wa homa ya nyani nje ya bara la Afrika unahitaji chanjo ya pamoja kwani hatua kama...
Shirika la Afya Duniani, WHO, haliamini kwamba mlipuko wa homa ya nyani nje ya bara la Afrika unahitaji chanjo ya pamoja kwani hatua kama vile usafi na ngono salama zitaisaidia kudhibiti kusambaa kwake.
Mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa virusi cha shirika hilo barani Ulaya, Richard Pebody, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kuna kiwango kidogo cha chanjo na dawa za kukabiliana na virusi vya homa hiyo.
Kauli ya Pebody inakuja wakati Kituo cha Udhibiti wa Maradhi cha Marekani kikisema kinapanga kutowa dozi za chanjo ya Jynneos kukabiliana na mripuko wa homa ya nyani.
Serikali ya Ujerumani ilisema hapo jana kwamba inatathmini njia za kugawa chanjo, huku Uingereza ikitowa chanjo hizo kwa wafanyakazi wa huduma ya afya. Mamlaka za afya Ulaya na Marekani zinachunguza wagonjwa zaidi ya 100 wanaoshukiwa kuambukizwa virusi hivyo, ukitajwa mripuko mkubwa kabisa wa homa hiyo nje ya bara la Afrika.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS