Waziri Mkuu aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta , asema Serikali inatafuta njia mbadala kupunguza gharama za maisha
HomeHabari

Waziri Mkuu aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta , asema Serikali inatafuta njia mbadala kupunguza gharama za maisha

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutok...

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

"Nawaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waiamini Serikali yao kuwa tunaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha tunapunguza gharama za maisha kwa wananchi,"  amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo jana (Alhamisi, Mei 5, 2022) katika kikao kilichofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye  ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Oysterbay, jijini Dar es Salaam ili kufanya tathmini ya bei ya mafuta na kuangalia namna gani Serikali inaweza kufanya ili kupunguza athari ya bei ya mafuta na kuleta unafuu wa gharama za maisha kwa Watanzania.

Waziri Mkuu amesema kikao hicho kimefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameagiza viongozi wa sekta husika wahakikishe wanatafuta suluhisho la kupanda kwa bei ya mafuta hata kama bei hiyo inaendelea kupanda duniani.

"Mheshimiwa Rais ameona changamoto wanayopitia Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, hivyo kikao hiki ni matokeo ya maagizo yake ya kuhakikisha sisi kama viongozi tunatafuta suluhisho la muda mfupi na la muda mrefu ili kukabiliana na changamoto hii," amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kuwa tayari Wizara ya Nishati imeanza kutafuta njia mbadala za uagizaji wa mafuta pamoja na kupunguza makato mengineyo ili kupunguza bei ya mafuta.

"Serikali inaangalia njia mbadala za uagizaji wa mafuta, kupitia kwa wazabuni wengine kama ambavyo imeshauriwa na wabunge na tayari mchakato huo umeanza, kwa kutathmini maombi 24 ambayo yaliwasilishwa kwa Wizara na sasa wamebaki wazabuni sita ambao wameingia hatua inayofuata. Inachokifanya Serikali hivi sasa ni kujiridhisha na uwezo wao wa kusambaza mafuta kulingana na mahitaji na taratibu zilizowekwa na Serikali,” amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bw. George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati, Bw. January Makamba, Makatibu Wakuu, pamoja na watendaji wakuu wa taasisi za EWURA, TPDC na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).


(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,





Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkuu aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta , asema Serikali inatafuta njia mbadala kupunguza gharama za maisha
Waziri Mkuu aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta , asema Serikali inatafuta njia mbadala kupunguza gharama za maisha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjyT1c5bijPGFFRidQJxkzJ45qrX6Dq5SfL5jiBGurr2fXAgbxdamhLkzN1s_wjxI8qJmdX5RnEoOIMcI1mIWTTzFjY8JQS1i_6h5jizyCBSRANGG9leyDEswDhH4eVna4mcSmo-zQ2CZJSmZlN8BYaodFCzJDKbCkBPt72mkitAVHQfrkp0dANXQNrg/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjyT1c5bijPGFFRidQJxkzJ45qrX6Dq5SfL5jiBGurr2fXAgbxdamhLkzN1s_wjxI8qJmdX5RnEoOIMcI1mIWTTzFjY8JQS1i_6h5jizyCBSRANGG9leyDEswDhH4eVna4mcSmo-zQ2CZJSmZlN8BYaodFCzJDKbCkBPt72mkitAVHQfrkp0dANXQNrg/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/waziri-mkuu-aitisha-kikao-cha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/waziri-mkuu-aitisha-kikao-cha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy