Dkt. Mchemba Akutana Na Wawekezaji Kutoka Uingereza Na Norway
HomeHabari

Dkt. Mchemba Akutana Na Wawekezaji Kutoka Uingereza Na Norway

 Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewahakikishia wawekezaji kutoka ...


 Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewahakikishia wawekezaji kutoka Uingereza na Norway kwamba Serikali itatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha uwekezaji wao hapa nchini kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji pamoja na vivutio kadhaa.
 
Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo Jijini Dar es Salaam
alipokutana na kufanya mazungumzo na kundi la wawekezaji kutoka nchini Uingereza na Norway, wanaotaka kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa nchini.
 
Ujio wa wawekezaji hao wanaotaka kuwekeza kwenye sekta za kilimo, nishati, uchimbaji na uchakataji madini, ujenzi wa miundombinu mbalimbali, ni matunda ya ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoifanya katika nchi za Ubelgiji na Nchi za Kiarabu hivi karibuni
 
Dkt. Nchemba aliwahakikishia wawekezaji hao tarajiwa, kwamba Serikali itaendelea kuboresha sera za uwekezaji na kuwatoa hofu kwamba Serikali ina sera za uwekezaji za uhakika, za kuvutia na zinazotabirika ili iweze kushiriki kikamilifu katika biashara za kimataifa, kikanda na kukidhi soko la ndani.
 
Alisema kuwa amani na usalama vilivyopo nchini, upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kuwekeza, uwepo wa idadi kubwa ya walaji likiwemo soko la ndani na soko la ukanda, ni fursa nyingine itakayowawezesha wawekezaji hao kupata faida katika uwekezaji wao.
 
Wakizungumza katika kikao hicho, wawekezaji hao walipongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuhamasisha uwekezaji pamoja na kuweka mazingira mazuri na rafiki ya uwekezaji na ufanyaji biashara.
 
Walisema kuwa wamekuja nchini kukutana na wadau zikiwemo Wizara na Taasisi mbalimbali ili kujifunza zaidi namna watakavyowekeza mitaji na teknolojia kwenye sekta za kilimo, uzalishaji wa umeme, uchakataji madini, mafuta na gesi.
 

Mwenyekiti wa wawekezaji hao Bw. Lanre Akinola, alisema kuwa katika miaka michache ijayo, Tanzania inatabiriwa kuwa itakuwa na uchumi imara na wenye nguvu zaidi kutokana na kutarajia kupata wawekezaji wengi kutoka Uingereza na Norway, hatua itakayo kuza uchumi pamoja na kuzalisha ajira kwa wananchi.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Mchemba Akutana Na Wawekezaji Kutoka Uingereza Na Norway
Dkt. Mchemba Akutana Na Wawekezaji Kutoka Uingereza Na Norway
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifs8DqAQE50jppmUMiGoi9HIqoH23omY-cUrtz2O41kKFoOrvl20U7Kv2Oi8JcVmunghXGlL9Mh3PuSg7Zm1-hZRWX-3i0qK-IbuQ7tJ_pioreuR97yMjdgnmsK_tCiNbaoXdbR6q0hgnVH0YWMKbnoqTl2q02THYPH4LHANecZ6yETpDi5vLu5PB1aw/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifs8DqAQE50jppmUMiGoi9HIqoH23omY-cUrtz2O41kKFoOrvl20U7Kv2Oi8JcVmunghXGlL9Mh3PuSg7Zm1-hZRWX-3i0qK-IbuQ7tJ_pioreuR97yMjdgnmsK_tCiNbaoXdbR6q0hgnVH0YWMKbnoqTl2q02THYPH4LHANecZ6yETpDi5vLu5PB1aw/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/dkt-mchemba-akutana-na-wawekezaji.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/dkt-mchemba-akutana-na-wawekezaji.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy