Wanaokwamisha Operesheni Ya Anwani Za Makazi Kuchukuliwa Hatua
HomeHabari

Wanaokwamisha Operesheni Ya Anwani Za Makazi Kuchukuliwa Hatua

 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima kuhakikisha anaw...


 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima kuhakikisha anawachukulia hatua wale watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika Mkoa huo

Akizungumza Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2022 jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Waziri Nape ameonesha kutokuridhishwa na kasi ya utekelezaji katika Mkoa huo unaoshika nafasi ya pili kutoka mwisho

“Hili la Operesheni ya Anwani za Makazi ni jambo letu sote, tuone shida ya kuwa mkiani, wanaotukwamisha washughulikiwe na kama kuna shida kwenye utekelezaji tuelezane tutatue kwa pamoja”, Amezungumza Waziri huyo

Waziri Nape amesisitiza kuwa uwekaji wa Anwani za Makazi sio zoezi la kawaida ni operesheni maalum iliyotangazwa na Rais, ambapo kukamilika kwake kutarahisisha kufanyika kwa sensa ya watu na makazi na ufikishaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima amekiri utekelezaji wa Operesheni hiyo bado haujaanza katika halmashauri tatu za Mkoa huo, ambazo ni halmashauri ya Korogwe mji, Korogwe vijijini na Kilindi kutokana na changamoto za kiutendaji

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Mfumo wa kielektoniki unaoingiza taarifa za wakazi na makazi unafanya kazi vizuri, na Wizara hiyo ipo tayari kutoa wataalamu kwenda kuongeza nguvu kwenye mkoa au halmashauri yeyote ambayo ina uhitaji.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wanaokwamisha Operesheni Ya Anwani Za Makazi Kuchukuliwa Hatua
Wanaokwamisha Operesheni Ya Anwani Za Makazi Kuchukuliwa Hatua
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj05sTCubDyM0bxM53uE40QT8eBScHE7SFPMpoeeyKaOFXxIVXndbN0mdL1DolEGvkyg2EMNhgA1j-wG00zNVXYgeFfTUNYORLB-fi7j8Z76ut6vQqFz0mp1yCkppYIR3OrpyITKCjg1IxI5cdBksESgdE0WYbkecoPY9_Dx81Z5jqOk1lzoX-YmHw8Ig/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj05sTCubDyM0bxM53uE40QT8eBScHE7SFPMpoeeyKaOFXxIVXndbN0mdL1DolEGvkyg2EMNhgA1j-wG00zNVXYgeFfTUNYORLB-fi7j8Z76ut6vQqFz0mp1yCkppYIR3OrpyITKCjg1IxI5cdBksESgdE0WYbkecoPY9_Dx81Z5jqOk1lzoX-YmHw8Ig/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/04/wanaokwamisha-operesheni-ya-anwani-za.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/04/wanaokwamisha-operesheni-ya-anwani-za.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy