Uongozi Wa Wizara Wawasisitiza Mabalozi Kufanya Kazi Kwa Bidii, Weledi
HomeHabari

Uongozi Wa Wizara Wawasisitiza Mabalozi Kufanya Kazi Kwa Bidii, Weledi

Na Mwandishi wetu, Dar Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umewaelekeza mabalozi kufanya kazi kwa bidi...

Treni Ya Abiria Yapata Ajali Eneo La Mkalamo, Mvave Wilaya Ya Pangani
Soko la Karume lateketea kwa Moto....Kamati kuundwa kuchunguza
Majaliwa: Ujenzi Wa Kiwanda Cha Mbolea Cha Itracom Ni Sahihi


Na Mwandishi wetu, Dar

Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umewaelekeza mabalozi kufanya kazi kwa bidii na weledi pamoja na kuweka maslahi ya Taifa mbele katika utekelezaji wa majukumu yao.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara Balozi Joseph Sokoine wakati walipokutana na mabalozi wanne walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 10, 2022. Uomngozi wa Wizara umekutana na mabalozi hao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mabalozi hao ambao ni miongoni mwa Mabalozi 23 walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Mei 22, 2021, wamekabidhiwa majukumu mbalimbali ya Wizara kwenye ngazi ya ukurugenzi.

Akiwaasa Mabalozi hao, Waziri Mulamula alisisitiza kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ni kiungo muhimu kati ya Serikali na dunia hivyo mawasiliano ya ndani na nje ya Wizara yafanyike kwa weledi na wakati kwa kuzingatia viwango vya  taifa na kimataifa. “Hii itasaidia sana kuendeleza diplomasia ya Tanzania hususan wakati huu ambapo Mheshimiwa Rais amefungua nchi kwenye nyanja zote” alisema.

Waziri Mulamula aliongeza kuwa matarajio ya Mheshimiwa Rais kwa kuwaapisha Mabalozi vijana ni kwamba wataimarisha utendaji kazi wa Wizara kuendana na kasi yake, hivyo ni muhimu kuchapa kazi bila urasimu. “Pale ambapo mnaweza kuweka ubunifu, fanyeni hivyo, leteni mawazo mapya milango yetu ipo wazi wakati wote ili tupige hatua”
 
Naye Katibu Mkuu wa Wizara aliongeza kuwa Mabalozi hao watapangiwa majukumu mengine ya kutoa mihadhara kwenye Chuo cha Diplomasia kwa watumishi wapya lakini pia Mabalozi hao wawe kiungo baina ya Taasisi zilizo chini ya Wizara na Taasisi nyingine Serikalini kama vile Chuo cha Diplomasia (CFR) na Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC)

Kwa mujibu wa viongozi hao, vyeo vya mabalozi hao ni: Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Director of Multilateral Cooperation), Balozi Macocha Tembele, Mkurugezi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Director of Government Communication) Balozi Mindi Kasiga, Mkurugenzi Kazi Maalum (Ambassador Special Duties), Balozi James Bwana pamoja na Mkufunzi Mwelekezi Mwandamizi  (Senior Directing Staff - Foreign) wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Balozi Noel Kaganda.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Uongozi Wa Wizara Wawasisitiza Mabalozi Kufanya Kazi Kwa Bidii, Weledi
Uongozi Wa Wizara Wawasisitiza Mabalozi Kufanya Kazi Kwa Bidii, Weledi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2AHZyf5eVBFbq96zPF1LpNfA5DF3WxLatK6rYtXluZo9gvFuBdsJdoMCmOA3WDP-0k_FbXXfYe_qplBqgnD84b0RuWoErY0DS-t5KQM_ka-djdHIAaW4FgbLgADj-gXX_oj0paB7qr9-unVbg-zEpNHUggEpFKW1rBJbiPKyix0Mm3uwxp-k1zT3Paw/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2AHZyf5eVBFbq96zPF1LpNfA5DF3WxLatK6rYtXluZo9gvFuBdsJdoMCmOA3WDP-0k_FbXXfYe_qplBqgnD84b0RuWoErY0DS-t5KQM_ka-djdHIAaW4FgbLgADj-gXX_oj0paB7qr9-unVbg-zEpNHUggEpFKW1rBJbiPKyix0Mm3uwxp-k1zT3Paw/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/04/uongozi-wa-wizara-wawasisitiza-mabalozi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/04/uongozi-wa-wizara-wawasisitiza-mabalozi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy