Taarifa Kwa Umma Mauaji Ya Wazee Shinyanga
HomeHabari

Taarifa Kwa Umma Mauaji Ya Wazee Shinyanga

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mauaji ya wazee   watatu   (Agnes Msengi miaka 84, Windila Saidi miaka 80 na Winfrida Gigil...

Mfalme Abdullah afariki dunia
EU yazindua miradi ya kupambana na ugaidi duniani
Wamarekani waadhimisha siku ya Martin Luther King Jr.


Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifaya mauaji ya wazee  watatu  (Agnes Msengi miaka 84, Windila Saidi miaka 80 na Winfrida Gigila miaka 80) waliouwawa  kwa kuchomwa moto  na wanakijiji wenzao kwa kile kinachodaiwa  kuwa wamekuwa wakishiriki vitendo vya kishirikina. Tukio hilo lilitokea tarehe 27/03/2022   katika kijiji cha Kisharita wilayani Iramba mkoani Singida.

Vitendo hivyo ni ukatili mkubwa ambao Serikali haiwezi kuvumilia na ni kinyume na sheria za nchi yetu na hata maagizo ya Mwenyezi Mungu katika dini zote zinapinga ukatili huu.

Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuchukua hatua za kutokomeza vitendo vya Ukatili hapa nchini kwa kusimamia utekelezaji wa; Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18-2021/22), Mkakati wa kutokomeza mauaji dhidi ya Wazee 2018/19 – 2022/2023, Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 20, Sera ya wazee 2003, na Uundwaji wa Mabaraza ya Wazee kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa.

Pamoja na hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na vyombo vya dola, nawaagiza Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwa karibu na wananchi ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuweza kuzitatua kwa wakati ikiwemo kuwaelimisha fursa zilizopo za kujikwamua kiuchumi, kuondokana na msongo wa mawazo na kukemea mila na desturi zinazochochea vitendo vya ukatili.

Pia nawasisitiza wazee wote nchini kupitia Mabaraza yao katika ngazi ya Vijiji/Mtaa na Kata kutoa taarifa za viashiria vyovyote vinavyohatarisha usalama wa wazee katika maeneo yao ili kuzuia vitendo vya ukatili.

Mwisho niiombe jamii, wanapoona matukio au viashiria vya vitendo vya ukatili watoe taarifa mapema kwa mamlaka zinazohusika kwa msaada wa haraka ili tuweze kuokoa maisha ya Wananchi wasio na hatia.

Imetolewa na:

 

Mhe. Dkt. Dorothy O. Gwajima (Mb)

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Taarifa Kwa Umma Mauaji Ya Wazee Shinyanga
Taarifa Kwa Umma Mauaji Ya Wazee Shinyanga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_Fcx67WD_ljkSu9QcR3WVOd0E8-kmX0b0YqJrwOrJ6R4-5xmYOAidTq0xDr-d9N7964Qwem02aVRCqBwv1vsR46-cXG6lceoOpRsVB_cljIDq-D9qwPCb1Gajf-5TEjWQF77CW3qfHvfqRUeZAWugzkkmdLZDHG6mh5uJ71aFlnZhDIkjpJpHcs-Msw/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_Fcx67WD_ljkSu9QcR3WVOd0E8-kmX0b0YqJrwOrJ6R4-5xmYOAidTq0xDr-d9N7964Qwem02aVRCqBwv1vsR46-cXG6lceoOpRsVB_cljIDq-D9qwPCb1Gajf-5TEjWQF77CW3qfHvfqRUeZAWugzkkmdLZDHG6mh5uJ71aFlnZhDIkjpJpHcs-Msw/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/taarifa-kwa-umma-mauaji-ya-wazee.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/taarifa-kwa-umma-mauaji-ya-wazee.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy