Makatibu Wakuu Sekta Ya Nishati Wa Eac Wakutana Jijini Arusha
HomeHabari

Makatibu Wakuu Sekta Ya Nishati Wa Eac Wakutana Jijini Arusha

Makatibu Wakuu wa sekta ya nishati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana  tarehe 10 Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania. Mk...

Stendi Mpya ya Mabasi Mbezi Luis kuanza kutumika February 25
Waziri Bashungwa Atoa Onyo Kwa Wanaotumia Vibaya Mitandao Ya Kijamii
Ndege Kudhibiti Nzige Longido Na Simanjiro- Waziri Mkenda


Makatibu Wakuu wa sekta ya nishati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana  tarehe 10 Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania.

Mkutano wa Makatibu Wakuu ulitanguliwa na mkutano wa Maafisa Waandamizi uliofanyika tarehe 8 na 9 Februari 2922. Mikutano hii mikutano ya awali kwaajili ya maandalizi ya Mkutano wa 15 Wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika kesho tarehe 11 Februari 2022.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ambaye ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Zanzibar, Dkt. Mngereza Miraji.

Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Makatibu Wakuu utapitia na kuandaa: Taarifa ya hali ya utekelezaji wa maagizo ya mikutano iliyopita; Hatua iliyofikiwa hadi sasa katika sekta za Nishati Umeme, Nishati Mafuta, na Nishati Jadidifu; pamoja na Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa na Kikanda ya Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Mkutano huo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wa Jamhuri ya Kenya, Maj. Gen. Dkt. Gordon Kihalangwa, CBS alieleza kuwa uhaba wa nishati ndani ya nchi zetu na jumuiya kwa ujumla huleta changamoto kwa wananchi wote na kushusha shughuli za uchumi na pato la taifa kwa ujumla. Hivyo, akasisitiza umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kutekeleza miradi ya nishati ya kitaifa na kikanda.

Vilevile akaeleza umuhimu wa sekta ya afya kupatiwa nishati ya kutosha na ya uhakika ili kuondoa changamoto za mara kwa mara zinazochangia kukosekana kwa huduma hizo.

“Huduma za mama na mtoto pamoja na huduma nyingine za afya ni muhimu zikazingatia upatikanaji wa nishati ili kupunguza matatizo yatokanayo na kukosekana kwa nishati ya uhakika kwa baadhi ya vifaa vinavyohitaji nishati ya umeme na gesi” alisema Dr. Gordon.

Mkutano huu umefanyika kwa njia ya mseto ambapo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda wameshiriki mkutano wa ana kwa ana isipokuwa Burundi, Rwanda na Sudan Kusini wameshiriki kwa njia ya mtandao.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Makatibu Wakuu Sekta Ya Nishati Wa Eac Wakutana Jijini Arusha
Makatibu Wakuu Sekta Ya Nishati Wa Eac Wakutana Jijini Arusha
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgIGah9RJVhZAtry9Impc0IDBpyBfIi8dDn-wErTDstVUKaGqZs2a4SjGPW5CwPwez_aP0RMwgTLZXZBmPG7aBTKa7ikzc2WeoFXNsNB4wGlMz9FSzdm7QGLttLmg9IFOS-_9nhlTwbBusyBh9-zWw-TycAs3liXWNm4d7rBXPiiUS-bn3QjglQDxVovQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgIGah9RJVhZAtry9Impc0IDBpyBfIi8dDn-wErTDstVUKaGqZs2a4SjGPW5CwPwez_aP0RMwgTLZXZBmPG7aBTKa7ikzc2WeoFXNsNB4wGlMz9FSzdm7QGLttLmg9IFOS-_9nhlTwbBusyBh9-zWw-TycAs3liXWNm4d7rBXPiiUS-bn3QjglQDxVovQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/makatibu-wakuu-sekta-ya-nishati-wa-eac.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/makatibu-wakuu-sekta-ya-nishati-wa-eac.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy