Watendaji Wa Halmashauri Ongezeni Ubunifu-Majaliwa
HomeHabari

Watendaji Wa Halmashauri Ongezeni Ubunifu-Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika halmashauri zote nchini waongeze ubujifu na waanzishe miradi inayotokana na asilim...


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika halmashauri zote nchini waongeze ubujifu na waanzishe miradi inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vinavyohitaji mikopo hiyo ili viweze kupata maendeleo.

Mheshimiwa Majaliwa alitoa kauli hiyo jana (Jumapili, Januari23, 2022) wakati akikabidhi pikipiki na guta kwa kikundi cha vijana kilichonufaika na mkopo wa asilimia 10 kutoka halmashauri ya Hanang’ akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Manyara.

Alisema kuwa kitendo cha kuwakusanya vijana na kuwatafutia jambo la kufanya na lenye tija ni hatua nzuri kwa sababu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza viongozi kuwa na maono ya mbali yanayoangalia Watanzania na mahitaji yao.

Akizungumza kwa niaba ya vijana walionufaika na mkopo huo, Damian Kalist alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba kupitia halmashauri ya wilaya ya Hanang’ ambayo ilitoa shilingi milioni 385 kwa vikundi 87.

“Mkopo huu ni nafuu na umetuwezesha kuondokana na mikopo kandamizi yenye riba kubwa iliyokuwa ikitolewa na baadhi ya taasisi mbalimbali za kifedha. Mikopo hii imetusaidia kutuinua kiuchumi na kutuongezea pato la familia na nchi kwa ujumla.”

Alisema kuwa kupitia mikopo hiyo wameweza kupata ajira binafsi pamoja na kutoa ajira kwa vijana wengine, hivyo kuwafanya vijana kuondokana na utegemezi wa kipato.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa alikagua ujenzi wa vyumba vinne ya madarasa katika Shule ya Sekomdari ya Wasichana ya Nangwa, ambapo aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kusimamia maelekezo ya ilani ya Chama cha Mapinduzi  ya kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anakwenda shule.

“Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametafuta fedha na amesambaza katika wilaya zote nchini, hapa Nangwa mmepata shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa haya manne na yana madawati ndani, viwango vya majengo haya ni bora kabisa.”

Alisema kuwa Wilaya ya Hanang’ imenufaika kwa kujengewa madarasa mapya 92 ambayo yatawawezesha watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kuanza masomo yao kwa pamoja. “Hii ni nia njema ya Rais wetu, anawapenda Watanzania na watoto wa kitanzania.”

Pia, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ afuatilie watoto wote wenye umri wa kwenda shule lakini hawaendi shule. “Lazima kila mtoto wa kitanzania aliyefikia umri wa kwenda shule apate elimu.”

Mheshimiwa Majaliwa aliongeza kuwa nia ya Mheshimiwa Rais Samia ni kuwafikia watanzania, kusikiliza kero na kuwahudumia. “Mheshimiwa Rais amejikita katika maeneo ambayo yanagusa maisha ya Watanzania ikiwemo maji, elimu, barabara, afya na umeme”

Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nangwa, Mwalimu Adelina Manya alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kuwapa fedha za ujenzi wa madarasa hayo manne kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19.

Alisema madara hayo yameondoa changamoto ya upungufu wa miundombinu ya vyumba vya madarasa shuleni hapo. Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1976 na ina tahasusi sita ambazo ni HKL, HGL, HGE, CBG, HGK na PCB zenye jumla ya wanafunzi 596, kati yao kidato cha tano ni 349 na kidato cha sita ni 247.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Watendaji Wa Halmashauri Ongezeni Ubunifu-Majaliwa
Watendaji Wa Halmashauri Ongezeni Ubunifu-Majaliwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjHOvoQWJzbKpG4Fy1PmckmGIt3Sn9_0m9lnXKMt_OpNE2oPpwxmiqdMlyP2jb6bEx7HvDFuxM2CRmADcH0WDHXJ3xqd1kNWBLBDX9r48OZs_yFfUdweegLTpwnKx1Pl7T7kwwb2OseuBqItb4XG4cLP3wdX3RKu2dw6fJtHEvL1KdovOzj0A_QyqBj2A=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjHOvoQWJzbKpG4Fy1PmckmGIt3Sn9_0m9lnXKMt_OpNE2oPpwxmiqdMlyP2jb6bEx7HvDFuxM2CRmADcH0WDHXJ3xqd1kNWBLBDX9r48OZs_yFfUdweegLTpwnKx1Pl7T7kwwb2OseuBqItb4XG4cLP3wdX3RKu2dw6fJtHEvL1KdovOzj0A_QyqBj2A=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/watendaji-wa-halmashauri-ongezeni.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/watendaji-wa-halmashauri-ongezeni.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy