Serikali Kulinda Maslahi Ya Wanahabari
HomeHabari

Serikali Kulinda Maslahi Ya Wanahabari

Na Immaculate Makilika na Prisca Ulomi, Mwanza Serikali imesema imedhamiria kulinda maslahi ya waandishi  wa habari nchini kwa kutatua c...


Na Immaculate Makilika na Prisca Ulomi, Mwanza

Serikali imesema imedhamiria kulinda maslahi ya waandishi  wa habari nchini kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakakabili.

Hayo yamesemwa  na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye , jijini Mwanza katika Uwanja wa Nyamagana wakati aliposhiriki katika tukio  la kuaga miili ya wanahabari 5 waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea jana  Januari 11, 2022 katika Wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu wakati wakielekea kwenye ziara ya kukagua miradi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel.

Mhe. Nape amewataka waajiri wa waandishi wa habari waliopata ajali na kufariki katika ajali hiyo kuwalipa maslahi yao kwa familia za marehemu.

“Natoa siku 7 kwa waajiri wote  kuanzia leo kulipa haki za wanahabari waliofariki na taarifa za uthibitisho wa malipo iwasilishwe kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza” alisisitiza Waziri Nape

Aidha, Waziri alisema kuwa Serikali itapitia upya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo ili kuboresha maslahi ya Wanahabari nchini.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza tupitie mapungufu ya sheria hiyo na kurekebisha ,  mimi nitahakikisha  nalinda uhuru na haki zenu ziko salama mikononi mwa Rais Samia, nami nitasimamia kwa kuwa sasa nimerudi nyumbani kusimamia sheria hii na tutahakikisha haki zenu zinalindwa kwa vile mimi ni muasisi wa sheria hii” Alisisitiza Waziri Nape.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Mhe. Mhandisi Gabriel alisema kuwa huu umekua msiba wa Taifa na Viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  wametuma salamu za pole kwa wafiwa na wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

Aidha, aliongeza kuwa Mkoa wa Mwanza umepata pigo kubwa na watahakikisha viongozi wa Mkoa huo wanaendelea  kutoa ushirikiano kwa wanahabari nchini ili kusaidia waendelee kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Wanahabari  watano waliofariki katika ajali hiyo ni Abel Ngapemba, Afisa habari wa Mkoa wa Mwanza, Steven Masengi, Afisa habari Wilaya ya Ukerewe na Husna Milanzi mwandishi wa ITV, Johari Shani mwandishi wa Uhuru digital na Anthony Chuwa mwandishi wa kujitegemea.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Kulinda Maslahi Ya Wanahabari
Serikali Kulinda Maslahi Ya Wanahabari
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEisYBX0345Gd2UPklIzxTo_rzHTPIVp28E0T78JOjhRAPkVjvm0w4LKSgc8kgnRmoNoLHqusRpUugwtUwkarR-jXpIEvZopK99eTNa5kd-Agq44CzeuwkWLd3gUsKdOy77X4e6IBeaooC1OLzf_3iqHrmf55YkxCXOqetNxLYPADWyu62iUM1C2Hr8LSg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEisYBX0345Gd2UPklIzxTo_rzHTPIVp28E0T78JOjhRAPkVjvm0w4LKSgc8kgnRmoNoLHqusRpUugwtUwkarR-jXpIEvZopK99eTNa5kd-Agq44CzeuwkWLd3gUsKdOy77X4e6IBeaooC1OLzf_3iqHrmf55YkxCXOqetNxLYPADWyu62iUM1C2Hr8LSg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/serikali-kulinda-maslahi-ya-wanahabari.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/serikali-kulinda-maslahi-ya-wanahabari.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy