Watu 14 wakiwamo waandishi wa habari saba wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa ...
Watu 14 wakiwamo waandishi wa habari saba wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo
Ameongeza kuwa majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa, watatu wamefariki dunia na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 14.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS