Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili TALIRI, DUCE, LATRA, MNH, TICD, NIT & WI
HomeHabari

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili TALIRI, DUCE, LATRA, MNH, TICD, NIT & WI

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jins...


TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Hospitali ya Taifa ya Mhimbili (MNH), Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT), na Chuo cha Maji (WI), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 08 - 10 Januari, 2022 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.      Usaili utafanyika   kuanzia tarehe 08-10 Januari, 2022 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili;  muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii.     Usaili wa Mchujo (kuandika) kwa kada zote utafanyika tarehe 08 Januari, 2022, na usaili wa Mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 10 Januari,

iii.   Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa, kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka, kutakasa mikono, kuvaa mavazi rasmi yanayoruhusiwa kazini  na pia inashauriwa kuvaa mavazi mazito kutokana na hali ya hewa ya ubaridi kwa kipindi hicho jijini Dodoma.

iv.    Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

v.   Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria; Msailiwa ambaye atakosa kitambulisho kimojawapo kati ya vilivyotajwa hataruhusiwa kufanya usaili;

vi.    Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

vii. Wasailiwa watakaowasilisha Hati za Ushuhuda wa ushiriki mafunzo (Testimonials), Hati za Matokeo ya muda mfupi (Provisional Results), Taarifa za Matokeo (Statement of results), Hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

viii.  Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

ix.    Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

x.     Kwa waombaji      waliosoma    nje   ya   Tanzania   wahakikishe   vyeti   vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);

xi.    Waombaji   kazi   ambao   majina   yao   hayakuonekana   katika   tangazo   hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.  Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xii.  Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

xiii.  Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti  zao  na  kunakili  namba  ya  mtihani  kwa  kuwa  namba  hizo hazitatolewa siku ya usaili.

==>> BOFYA HAPA KUSOMA TANGAZO RASMI LIKIWA PAMOJA NA MAJINA.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili TALIRI, DUCE, LATRA, MNH, TICD, NIT & WI
Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili TALIRI, DUCE, LATRA, MNH, TICD, NIT & WI
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgGHVYe7dB2o1sGItKMTCXbvgYPzGQ_T1-d8tGk3zkFRNmfHkeNCtXtLGqcVCfOLiPfytxF-Emj1FBkYpNzg4PPkTCzmKSDteBRP2GfkmXTFLjuPTJqq_M1eHg8hQzMuN_c9Zjtqdxtmou3B_TteKDQeIEbG8VyiTdJzycoa0DRFLnblDOtE5si8dJGDA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgGHVYe7dB2o1sGItKMTCXbvgYPzGQ_T1-d8tGk3zkFRNmfHkeNCtXtLGqcVCfOLiPfytxF-Emj1FBkYpNzg4PPkTCzmKSDteBRP2GfkmXTFLjuPTJqq_M1eHg8hQzMuN_c9Zjtqdxtmou3B_TteKDQeIEbG8VyiTdJzycoa0DRFLnblDOtE5si8dJGDA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/tangazo-la-kuitwa-kwenye-usaili-taliri.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/tangazo-la-kuitwa-kwenye-usaili-taliri.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy