Rais Samia avunja bodi ya bandari, Shirika la Meli
HomeHabari

Rais Samia avunja bodi ya bandari, Shirika la Meli

Rais  Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na...


Rais  Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza wizara kuichukulia hatua bodi ya manunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa kampuni ‘hewa’.

Maamuzi ya Rais Samia leo Dis. 4 yanafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini.

Dau hili lenye thamani ya Sh bilioni 438.8 lilisainiwa mjini Mwanza Jun. 15, 2021 nakushuhudiwa na Rais Samia. Hata hivyo timu iliyohusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Askari kutoka kikosi ya wanamaji, na wataalamu kutoka MSCL ilibaini kuwa YÜTEK haikuwa na uwezo wa kifedha wala wataalamu kutekeleza mkataba huo.

“Nimeagiza Waziri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuvunja mkataba huo… hata hivyo uwezo wangu ni kuvunja bodi hivyo wenyeviti wote wawili nimewaondoa,” alisema Rais Samia wakati akizindua maboresho ya gati za Bandari ya Dar es Salaam.

Rais Samia amesema mkandarasi huyo alikuwa ameweka wakala nchini aliyekuwa anufaike kati ya Dola za Marekani milioni 1.9 hadi 2 kwa kila meli itakayo jengwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi, Mkandasi huyo hana eneo la kujenga meli (shipyard) badala yake wao ni madalali wa kutafuta kazi na kutoa kwa kampuni zingine. Pia ilibainika kwamba uwezo wa kampuni kifedha ni mdogo mno.

Wasifu na uwezo wake katika ujenzi ni wa mashaka kwani haipo hata kwenye orodha ya wajenzi wa meli inayotolewa na umoja wa wajenzi wa meli Uturuki. “Hili ndio liliotuthibitishia kwamba hawa ni madalali. hawakuwa na watu wenye sifa na vifaa vya kujenga meli. hadi sasa kampuni hiyo haijafanya lolote,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amehoji ikiwa uwezo wa kampuni hiyo ulikuwa ni kutengeneza boti ndogo.

“Tujiulize tenda hii ilitolewa na bodi husika ya wizara ama shirika. Shirika linabodi ya wakurugenzi ambao wamepitisha tenda hii lakini pia mkandarasi alifanyiwa due diligence. Sasa haya tumeyabaini hivi karibuni, huko nyuma yametokea mangapi?” alihoji nakutaka tenda bodi iliyohusika, bodi ya wakurugenzi kuwajibishwa.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia avunja bodi ya bandari, Shirika la Meli
Rais Samia avunja bodi ya bandari, Shirika la Meli
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjfVvtg6CXDfCZyZFNP4QGFME31j5DVeDrZ8HjIZNxC7nJ4yXTSn5EVRiTptkZlasZEB0eT4-skdkqItTvEWDYhUs25bd7OYoxj6_D85ImlR_FyIfCGib2FeBzCtvqdsFLM2AgnoO3L-rW-rrMrLIpCAEfCHuitPYYAz90v2qNU39JAksX4qr_2JGsDCw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjfVvtg6CXDfCZyZFNP4QGFME31j5DVeDrZ8HjIZNxC7nJ4yXTSn5EVRiTptkZlasZEB0eT4-skdkqItTvEWDYhUs25bd7OYoxj6_D85ImlR_FyIfCGib2FeBzCtvqdsFLM2AgnoO3L-rW-rrMrLIpCAEfCHuitPYYAz90v2qNU39JAksX4qr_2JGsDCw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/rais-samia-avunja-bodi-ya-bandari.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/rais-samia-avunja-bodi-ya-bandari.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy