NEMC Kushirikiana Na Wawekezaji Katika Miradi Yote Ya Kimkakati Ili Kuepuka Uharibifu Wa Mazingira - Dkt. Gwamaka
HomeHabari

NEMC Kushirikiana Na Wawekezaji Katika Miradi Yote Ya Kimkakati Ili Kuepuka Uharibifu Wa Mazingira - Dkt. Gwamaka

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka, amefanya ziara katika eneo linalotarajiwa kuje...

Tanzania Yashiriki Mkutano Wa Kamati Ya Mawaziri Wa Sheria Wa SADC
Airtel Tanzania Yatoa Gawio La Sh.bilioni 122 Kwa Miaka Miwili
Majaji watakikwa kuzijua sheria za Afrika Mashariki


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka, amefanya ziara katika eneo linalotarajiwa kujengwa mradi wa kituo kitakachopokea na kuhifadhi mafuta katika Kijiji cha Chongoleani Tanga. 


Lengo kuu la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Sheria, Taratibu na Kanuni za utunzaji wa mazingira katika hatua ya awali ya utekelezaji wa mradi huo.  Ziara hii ni moja ya utekelezaji wa ajenda kubwa ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan.


“Sisi kama NEMC ni lazima tutimize maagizo ya Mhe. Rais na moja ya mikakati ambayo tumeiweka ni kuanza kuwa na mtazamo chanya kwa maana ya kwamba wawekezaji wote hasa kwenye miradi ya kimkakati tunatakiwa kuwa nao kuanzia hatua ya awali ya utekelezaji wa mradi ili kutambua nini wanakifanya na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhakikisha wanaenda sambamba na Sheria ya Mazingira. Mradi wa bomba la mafuta ni mradi mmojawapo ya kimkakati katika nchi yetu utakaoleta tija na faida kwa nchi ”


Pia Dkt. Gwamaka amewapongeza viongozi wa mradi wa EACOP kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kushirikiana na jamii inayozunguka mradi ikiwa ni pamoja na kuwalipa fidia na kuwashirikisha katika kila hatua kadri mradi unavyoendelea kutekelezwa.


Afisa Mazingira kutoka NEMC Bi. Dalia Charles ametoa rai kwa wananchi wa Chongoleani na nchi kwa ujumla kuwa Baraza limejiridhisha na mikakati mahsusi iliyowekwa na wawekezaji kudhibiti mwanya wowote wa athari inayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi, hivyo basi mradi huo hautakuwa na madhara  na una manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. 


Aidha Diwani wa kata ya Chongoleani Bw. Mwaveso Kassimu Mbega ameuhakikishia umma kua mradi huo umepokelewa vizuri na wananchi wa Kata hiyo ambao wameridhika kuachia maeneo yao ili mradi ujengwe na kuishukuru Serikali kupeleka mradi katika eneo hilo, lakini pia amewaomba wananchi wa Chongoleani kuwa na imani na mradi huo kwani Serikali ina nia njema na wananchi wake haiwezi kupeleka mradi wenye madhara, mradi huo unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa wananchi na kwa serikali kwa ujumla.


Naye Mtendaji wa Kata ya Chongoleani Bw. Mohamedi Omari Salimu amesema kumekuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka mradi huo. Wananchi wamepata stahiki zao ikiwa na kulipwa fidia na kumekua na taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya mradi huo




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: NEMC Kushirikiana Na Wawekezaji Katika Miradi Yote Ya Kimkakati Ili Kuepuka Uharibifu Wa Mazingira - Dkt. Gwamaka
NEMC Kushirikiana Na Wawekezaji Katika Miradi Yote Ya Kimkakati Ili Kuepuka Uharibifu Wa Mazingira - Dkt. Gwamaka
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiRXrFb0PgZ-asefoxRxmtH_9YBQU-8FYzrgXcdOSYXMxC2h9t7TAUib5Xl3aJ3ylxKbmHnSpulXxFJJL0Q6aax8QaauRZe6vRwPgEwBWuNAOBpMXUjdu6OlVoM7oaF7gDKFKZs3njp2mlVpWHCTNwvvIi-_3o12tpCJc7Kx6PyEl-JEAFSOp-ADyigWQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiRXrFb0PgZ-asefoxRxmtH_9YBQU-8FYzrgXcdOSYXMxC2h9t7TAUib5Xl3aJ3ylxKbmHnSpulXxFJJL0Q6aax8QaauRZe6vRwPgEwBWuNAOBpMXUjdu6OlVoM7oaF7gDKFKZs3njp2mlVpWHCTNwvvIi-_3o12tpCJc7Kx6PyEl-JEAFSOp-ADyigWQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/nemc-kushirikiana-na-wawekezaji-katika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/nemc-kushirikiana-na-wawekezaji-katika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy