Rais Samia Anaamini Takukuru Itamsaidia Kujenga Taifa Ambalo Wananchi Watanufaika Na Rasilimali Zilizopo
HomeHabari

Rais Samia Anaamini Takukuru Itamsaidia Kujenga Taifa Ambalo Wananchi Watanufaika Na Rasilimali Zilizopo

Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ...


Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anaamini kuwa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) itamsaidia kujenga taifa ambalo wananchi anaowaongoza watanufaika na uwepo wa rasilimaliwatu na rasilimali za umma zilizopo pasipo kuombwa wala kutoa rushwa.

Waziri Mchengerwa amesema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021 wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) uliofanyika jana jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa amesema, mapambano dhidi ya rushwa yamejikita katika misingi ya Utawala Bora, hivyo amewataka viongozi wa TAKUKURU kujipanga katika mapambano dhidi ya rushwa ili taifa liwe na watumishi na taasisi za umma zinazotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.

Ameongeza kuwa, moja ya vinyemelea vya rushwa katika Taasisi za Umma ni urasimu wa utoaji wa huduma hivyo kama utoaji wa huduma utazingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo hakuna mwananchi atakayeshawishika kutoa rushwa.

“Anayekwenda kusajili biashara yake BRELA akijua kwamba huduma ya usajili inapatikana ndani ya siku moja na ndani ya muda huo akafanikiwa kusajili biashara yake, hatakuwa na wazo la kutoa rushwa,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Katika kutekeleza jukumu la kumsaidia Mhe. Rais kuongoza mapambano dhidi ya rushwa, Mhe. Mchengerwa amewataka watendaji wa ofisi yake kujipanga vema katika kusimamia misingi ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kwa kufanya hivyo taifa litakuwa limefanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa.

Ili kuongeza ufanisi kiutendaji, Mhe. Mchengerwa ameitaka TAKUKURU kushirikiana na Idara ya Ukuzaji wa Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhakikisha wanapata takwimu sahihi ya namna ambavyo huduma katikaTaasisi za Umma zinatolewa kwa wananchi, na kwa taasisi zitakazobainika kutotoa huduma bora hatua stahiki zichukuliwe kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni, amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kufungua kikao kazi cha taasisi yake ambacho kitasaidia kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha utendaji kazi wa TAKUKURU.

Sanjali na hilo, amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa na kwa kutoa maelekezo ya mara kwa mara yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa taasisi yake.

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021 wa Viongozi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) uliofunguliwa rasmi leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa utafanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 25 hadi 27, 2021.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia Anaamini Takukuru Itamsaidia Kujenga Taifa Ambalo Wananchi Watanufaika Na Rasilimali Zilizopo
Rais Samia Anaamini Takukuru Itamsaidia Kujenga Taifa Ambalo Wananchi Watanufaika Na Rasilimali Zilizopo
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjBlTu_uoy05OWcA3eETyRpNM8AYXI6Ju50QG0qgk9r1O9sk6eI_-4zSBHz49nqpRPET-YPw2zVwN22K1vVri7xfOWKvsvP_zcPkBByTbSPBkV643RZLCHBed-w2D6706rfZ6OmwUtyJoVJumyZzqq7VYArx6f6cVvggEgSlSJgUndsS-2I0rRbA4fOBA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjBlTu_uoy05OWcA3eETyRpNM8AYXI6Ju50QG0qgk9r1O9sk6eI_-4zSBHz49nqpRPET-YPw2zVwN22K1vVri7xfOWKvsvP_zcPkBByTbSPBkV643RZLCHBed-w2D6706rfZ6OmwUtyJoVJumyZzqq7VYArx6f6cVvggEgSlSJgUndsS-2I0rRbA4fOBA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/rais-samia-anaamini-takukuru-itamsaidia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/rais-samia-anaamini-takukuru-itamsaidia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy