Mbarawa: Siku Zahesabika Kwa Wasimamizi Wa Mizani
HomeHabari

Mbarawa: Siku Zahesabika Kwa Wasimamizi Wa Mizani

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amewataka wasimamizi na wafanyakazi wa mizani nchini kujitafakari kuhusu mienendo y...


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amewataka wasimamizi na wafanyakazi wa mizani nchini kujitafakari kuhusu mienendo yao ya utendaji kazi kabla hatua stahiki hazijachukuliwa.

Ametoa angalizo hilo Novemba 19, 2021 jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa makao makuu ya Wakala wa Barabara (TANROADS) na kueleza kuwa pamoja na kufungwa mifumo ya kamera za CCTV bado kumekuwa na malalamiko ya vitendo vya rushwa kwa watumishi katika mizani zilizoko maeneo mbalimbali nchini.

“Ni aibu na ni jambo la hovyo mtumishi wa mizani anaenda kuchukua rushwa hadharani na hajali uharibifu unaoendelea wa barabara zetu, huu ni mtandao unaoendelea kuanzia wa chini hadi wa juu, nawaambia na kuwatahadharisha kuwa siku zenu zinahesabika na nitawatoa siku za karibuni”, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amewataka TANROADS kutoa elimu ya kutosha kwa wasafirishaji wote nchini ili kuwasaidia kufahamu haki na wajibu wao katika kusaidia kulinda miundombinu ya barabara na kupunguza malalamiko ya mara kwa mara.

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa TANROADS kuhakikisha barabara kuu zinazounganisha mikoa yote nchini zinawekwa vivuko vya waenda kwa miguu au madaraja ya juu pahala panapostahili ili kupunguza idadi ya vifo vya watumiaji wa barabara.

“Tukumbuke kuwa tunajenga barabara si kwa ajili ya magari tu bali na watembea kwa miguu kama moja ya watumiaji wa barabara hizi, Nalisema hili kwa kuwa nimekuwa nikipokea malalamiko kadhaa hasa barabara ya Kimara – Kibaha nendeni mkaweke vivuko”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Awali akitoa taarifa ya Wakala, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Rogatius Mativila, amemueleza Waziri huyo kuwa katika mwaka huu wa fedha 2021/22 imejipanga kutekeleza miradi yote ya kimkakati kwa wakati na ubora unaotakiwa ambapo kiasi cha shilingi bilioni 897.656 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na shilingi Bilioni 567.342 zitatumika katika matengenezo ya kawaida, matengenezo ya muda maalum, matengenezo sehemu korofi na matengenezo ya madaraja.

Ametaja miradi iliyopangwa kutekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi mpya wa barabara kuu kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 467.11 na barabara za mikoa zenye urefu wa kilometa 103.

Eng. Mativila ameongeza kuwa kwa upande wa madaraja, TANROADS itajenga na kukarabati madaraja 21 yaliyopo katika barabara kuu na ujenzi wa madaraja na makalvati makubwa 66 katika barabara za mikoa.

Waziri Prof. Mbarawa anaendelea na ziara yake jijini Dar es Salaam yenye lengo la kukagua miradi inayoendelea kutekelezwa pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mbarawa: Siku Zahesabika Kwa Wasimamizi Wa Mizani
Mbarawa: Siku Zahesabika Kwa Wasimamizi Wa Mizani
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEinrDu9XB4r4QTkV4Fhbw3WGFoJHIA49z-qDMvBY9W62NUbPbeBgr_AKD9E7NYsscwvU3KmvZruEnQ15PNuitnHaMkF4ZDOh2es1C_xgyo3ySAprfJh4nYO3eUEo0_dpjJ0UwpngsvzeN-hZdHjWhbbYh7ASyUygCNBAhNUXJW-8BYpwDVpxPhEO3U6hg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEinrDu9XB4r4QTkV4Fhbw3WGFoJHIA49z-qDMvBY9W62NUbPbeBgr_AKD9E7NYsscwvU3KmvZruEnQ15PNuitnHaMkF4ZDOh2es1C_xgyo3ySAprfJh4nYO3eUEo0_dpjJ0UwpngsvzeN-hZdHjWhbbYh7ASyUygCNBAhNUXJW-8BYpwDVpxPhEO3U6hg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/mbarawa-siku-zahesabika-kwa-wasimamizi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/mbarawa-siku-zahesabika-kwa-wasimamizi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy