Waziri Biteko Awataka Wafanyabiashara Wa Madini Kusajili Mikataba Na Wabia Wao Tume Ya Madini
HomeHabari

Waziri Biteko Awataka Wafanyabiashara Wa Madini Kusajili Mikataba Na Wabia Wao Tume Ya Madini

  Na Steven Nyamiti- WM WAFANYABIASHARA wa madini wametakiwa kuingia mikataba na wabia wao kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha mikataba ...

 


Na Steven Nyamiti- WM
WAFANYABIASHARA wa madini wametakiwa kuingia mikataba na wabia wao kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha mikataba hiyo inasajiliwa katika ofisi ya Tume ya Madini ili itambuliwe na Serikali.

Rai hiyo imetolewa leo Oktoba 6, 2021 na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko alipotembelea na kuzungumza na Wafanyabiashara Wakubwa na wadogo wa Madini (Dealers & Brokers) katika Soko Kuu la Madini ya Dhahabu mkoani Geita.

Dkt. Biteko ameagiza ubia wa wafanyabiashara wa madini na wawekezaji usajiliwe kwenye ofisi za Serikali ili itambulike kisheria na kusaidia kutatua migogoro inapojitokeza kwa kudhulumiana au kupoteza uaminifu.

Amesema, wafanyabiashara Wakubwa na Wadogo wanatakiwa kuifanya kazi yao ipasavyo na kusimamia madini yasitoroshwe. Pia, kulipa kodi na tozo stahiki za Serikali hivyo kuwafanya watendaji kuweka nguvu kubwa katika kusimamia shughuli za madini.

Akizungumzia kuhusu uongezaji thamani madini, Dkt. Biteko amesema kuwa, Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza uongezaji thamani wa madini ufanyike hapa hapa nchini ili kulinda ajira za Watanzania na kuepusha Tanzania kuwa chanzo cha malighafi ya viwanda ya nchi za wenzetu.

"Kuanzia madini ya Vito, madini ya Dhahabu, hatumpi mtu leseni ya 'Dealer' mpaka awe na mashine 30 za kukata madini ili madini hayo yaongezwe thamani hapa ndani na si kusafilisha madini ghafi," amesisitiza Dkt. Biteko.

"Tuliamua kujenga viwanda vya kusafisha madini ili tusafishe madini ndani ya nchi. Hatuwezi kuwa na viwanda hapa halafu mtu akabeba madini akapeleka Uswisi kwenda kusafisha wakati hapa tunasafisha na viwanda vipo," ameeleza Dkt. Biteko.

Aidha, amesema Serikali inaunga mkono biashara na shughuli za madini ili wafanyabiashara na wawekezaji wafanye vizuri zaidi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Soko la Madini Geita, Situmaini Bigazaba ameipongeza Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Geita kwa kusimamia biashara ya madini na kutoa maelekezo mbalimbali ya taratibu za biashara ikiwemo Kanuni na Sheria zinazowalinda wafanyabiashara wa madini.

Waziri Dkt. Biteko amefanya ziara ya siku moja mkoani Geita ambapo amekutana na wadau mbalimbali wa madini kuzungumza nao na kutatua migogoro katika shughuli zao.

MWISHO


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Biteko Awataka Wafanyabiashara Wa Madini Kusajili Mikataba Na Wabia Wao Tume Ya Madini
Waziri Biteko Awataka Wafanyabiashara Wa Madini Kusajili Mikataba Na Wabia Wao Tume Ya Madini
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjeZEsAOCeqwhigaFao5Fy_GPnr5U3Zl3_I7GjM6xaRoWUFDsqpE_LjpADXlODSg4L7IhxtW6I-k4Np3Y3pU_Z4NhWP6_tSKrZ69V2BbVWPB8ajh-A0Y9XvZhkxgV4uTuzdFwgljG3gYNDvRJLrELwtlhilygmsEkIDrk6LsIClE9VDwHLXD-7sHjBqHg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjeZEsAOCeqwhigaFao5Fy_GPnr5U3Zl3_I7GjM6xaRoWUFDsqpE_LjpADXlODSg4L7IhxtW6I-k4Np3Y3pU_Z4NhWP6_tSKrZ69V2BbVWPB8ajh-A0Y9XvZhkxgV4uTuzdFwgljG3gYNDvRJLrELwtlhilygmsEkIDrk6LsIClE9VDwHLXD-7sHjBqHg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/waziri-biteko-awataka-wafanyabiashara.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/waziri-biteko-awataka-wafanyabiashara.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy