Wanawake Ni Muhimu Katika Maendeleo Ya Taifa: Rais Putin
HomeHabari

Wanawake Ni Muhimu Katika Maendeleo Ya Taifa: Rais Putin

Na. WAMJW-St. Petersburg, Urusi Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonesha kuwa wanawake ni muhimu katika maendeleo ya taifa lolote kulingan...


Na. WAMJW-St. Petersburg, Urusi
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonesha kuwa wanawake ni muhimu katika maendeleo ya taifa lolote kulingana na asili ya majukumu yao wanayoyafanya hasa katika malezi kwa mtoto.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima mara baada ya kushiriki kwenye Kongamano la tatu la Wanawake lililofunguliwa na Rais huyo na kuhudhuriwa viongozi wa mataifa mbalimbali nchini hapa.

Dkt. Gwajima amesema kuwa Rais huyo  amebainisha kwamba ni namna gani wanawake ni muhimu katika hatua za awali za malezi na makuzi ya mtoto ambapo mambo mengi ya msingi ambayo mtoto anapaswa kupatiwa katika msingi wa makuzi yake mwanamke anahusika moja kwa moja kwani muda mwingi anakuwa na mtoto katika malezi yake.

“Rais Putin amerejea mfano wa taifa la Urusi ambalo linafanya vizuri katika kuwapa nafasi  Wanawake waweze kushiriki kwenye maendeleo ya nchi na jinsi gani Wanawake wanapewa fursa katika nyanja zote za maendeleo la taifa kwa sekta zote.

“Tumeweza kujifunza kwamba hata sisi nyumbani muelekeo anaochukua Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwajenga na kuwawezesha wanawake katika nyanja zote wasiachwe nyuma ni muelekeo sahihi kwani imejionesha katika nchi kubwa kimaendeleo duniani ziliweza kuona msingi mzima wa nafasi ya mwanamke katika kuchangia maendeleo ya jamii”.

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa wanawake ndio wanaoleta Taifa kuwa na sura fulani na  tabia nyingi wanazorithi watoto wetu wakiwa wadogo zinabaki katika kumbukumbu zao na ndizo zinazojenga taifa mbele ya safari.

Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa Rais Putin amewapa changamoto hivyo wanaporudi Tanzania lazima wakafanyie kazi kwa nguvu ili dhamira ya Mhe. Rais Samia ya kuwatoa wanawake wengi ambao wapo nyuma na hawana nafasi nzuri kimaendeleo  wapande juu na wachangie maendeleo ya taifa.

Hata hivyo Dkt. Gwajima ameahidi kutokana na Kongamano hilo Serikali ya Tanzania itajipanga kuwa na kongamano la Wanawake kupitia Majukuwaa  ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ambayo yapo kwenye ngazi za halmashauri hadi Mikoa ili kuweza kujiandaa kwa miaka inayokuja kuwasilisha yatokanayo na kongamano hili na hata kuwaalika mwanawake wa mataifa mengine wafike Tanzania na kuona mafanikio yatakayofikiwa na wanawake wa Tanzania.

Wakati huo huo akizungumza na Kituo cha Runinga cha Serikali cha “Russia One” Dkt. Gwajima alibainisha kuwa Tanzania ipo salama kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19 na kwamba idadi ya maambukizi yamepungua huku akitolea mfano kati ya  tarehe 2  hadi 8 mwezi Oktoba Tanzania iliandikisha kesi mpya  77 na wagonjwa 171 ndio waliokuwa wamelazwa ukilinganisha na idadi ya watu waliopo na hivyo kuwaondoa hofu wananchi wa Urusi na kuwathibitishia mipaka ya Tanzania ipo wazi hivyo hamna haja ya kufungia ndege zao kuruka Tanzania na za Tanzania kuruka Urusi.

Kwa upande wa utalii Waziri huyo aliwathibitishia Urusi kuwa Tanzania inapokea idadi kubwa ya watalii  kutoka mataifa mbalimbani na kwamba idadi ya watalii kuanzia Mwezi Agosti 2020 hadi Februari, 2021 zaidi ya watalii laki moja (100,000) waliweza kuingia Tanzania na waliondoka wakiwa salama.

Akielezea kuhusu Madini Dkt. Gwajima alisema Tanzania ndio nchi Pekee duniani inayozalisha inayozalisha madini ya Tanzanite na ni moja ya vito adimu na yenye thamani ambayo huchimbwa  kaskazini mwa nchi katika eneo la Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara hivyo amewaalika wawekezaji kutoka nchini Urusi kuwekeza katika Sekta hiyo hususan kwenye Masuala ya uongezaji thamani wa madini hayo.

MWISHO.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wanawake Ni Muhimu Katika Maendeleo Ya Taifa: Rais Putin
Wanawake Ni Muhimu Katika Maendeleo Ya Taifa: Rais Putin
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjwPZvZpZk7Ya8JF3pVlpKbN8gP1-z_cUGAhVpXfys3q-r0KnJOHwTIonrSYt1YMy8BR2FjyBRr0J44j9Uzlm3qPbrZlsCV77ap66VX9jCO8mb2n-a8VFZIUUixnVv1AnzKqEyXM6ubnt1wQRCS-iZZTWYJIgjo3_jrbQm_9aXX4qLZe26rW1nPUTZyQw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjwPZvZpZk7Ya8JF3pVlpKbN8gP1-z_cUGAhVpXfys3q-r0KnJOHwTIonrSYt1YMy8BR2FjyBRr0J44j9Uzlm3qPbrZlsCV77ap66VX9jCO8mb2n-a8VFZIUUixnVv1AnzKqEyXM6ubnt1wQRCS-iZZTWYJIgjo3_jrbQm_9aXX4qLZe26rW1nPUTZyQw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/wanawake-ni-muhimu-katika-maendeleo-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/wanawake-ni-muhimu-katika-maendeleo-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy