Serikali Haitowavumilia Watumishi Wa Umma Watakaoshindwa Kutimiza Wajibu
HomeHabari

Serikali Haitowavumilia Watumishi Wa Umma Watakaoshindwa Kutimiza Wajibu

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan haitawavumilia watumi...

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan haitawavumilia watumishi wa umma watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“…Rais anahitaji kuona watumishi wa umma wakifanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili. Pia anataka kuona watumishi wakiwafuata wananchi katika maeneo yao ya makazi na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.”

Ameyasema hayo jana (Jumatano, Oktoba 6, 2021) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kipatimu wilayani Kilwa baada ya kutembelea Hosptali ya Mission ya Kipatimu akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.

Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi hao wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa pamoja na kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dkt. Kheri Kagya ahakikishe mtaalamu wa X-ray anapelekwa katika Hosptali ya Mtakatifu Martin iliyopo Kipatimu ili kuwapunguzia wananchi wa maeneo hayo kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Ametoa agizo hilo baada ya uongozi wa hospitali hiyo ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki kumueleza Waziri Mkuu kwamba hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa mtaalamu wa X-ray licha ya kuwa na kifaa hicho.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Dkt. Kagya ahakikishe hospitali hiyo ambayo kwa sasa ina daktari mmoja iongezewe daktari mwingine ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Christina Kasyama alisema hospitali hiyo ambayo inamilikiwa na Jimbo Katoliki la Lindi inafanya kazi kwa ushirikiano na Serikali kupitia mkataba wa huduma (PPP) na inahudumia wakazi takribani 50,000 wa Kilwa Kaskazini na maeneo ya jirani.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Haitowavumilia Watumishi Wa Umma Watakaoshindwa Kutimiza Wajibu
Serikali Haitowavumilia Watumishi Wa Umma Watakaoshindwa Kutimiza Wajibu
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhvWu_vsppJgcnP59vqXW1Q2G0_nBhWnqrjDwy6vAjV83lgK5SmJX47ret8h7nZmWK6hLCOKs27jdCJhpr4K-ISyA7MLAz3xeD7ZDY4V0WzTdqb8_vEGaRP1FKQVmTSMdNLUuIgB1RzYa0aBRfMz9nkhFf7uIs-uh0Tp7fAOs5UuayYdV2SXe4LHzonCg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhvWu_vsppJgcnP59vqXW1Q2G0_nBhWnqrjDwy6vAjV83lgK5SmJX47ret8h7nZmWK6hLCOKs27jdCJhpr4K-ISyA7MLAz3xeD7ZDY4V0WzTdqb8_vEGaRP1FKQVmTSMdNLUuIgB1RzYa0aBRfMz9nkhFf7uIs-uh0Tp7fAOs5UuayYdV2SXe4LHzonCg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/serikali-haitowavumilia-watumishi-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/serikali-haitowavumilia-watumishi-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy