Rais Samia Amuagiza Waziri Ummy Kutoa Bil. 1/= Ujenzi Hospitali Arusha
HomeHabari

Rais Samia Amuagiza Waziri Ummy Kutoa Bil. 1/= Ujenzi Hospitali Arusha

Rais Samia Suluhu Hassan, amuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, kutoa Sh...


Rais Samia Suluhu Hassan, amuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, kutoa Sh. bilioni moja kabla ya Novemba 30, mwaka huu, kwa ajili ya kuchangia ujenzi unaoendelea wa hospitali ya Wilaya ya Arusha.

Aidha, amekabidhi hundi ya Sh. bilioni 1.39 kwa vikundi 152 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Rais Samia alitoa agizo hilo Oktoba 17, 2021, baada ya kuzindua hosptali hiyo ya kisasa ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya sh. bilioni 2.5 ambazo zinatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.

“Nimefurahishwa sana kwa jinsi  ambavyo mmekusanya vizuri mapato yenu ya ndani na kujenga hospitali hii ya kisasa. Kwa sababu hii, nimemwagiza waziri wa TAMISEMI, Ummy, kuleta hapa kiasi cha sh. bilioni moja kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi huu ambao tayari wana majengo mawili ya kisasa yaliyokamailika,” alisema.

Rais Samia alisema licha ya kutoa fedha hizo, pia serikali kuu itatoa dawa na vifaatiba katika hospitali hiyo, ili wanachi waendelee kupata huduma bora za afya.

Katika hatua nyingine, Rais Samia aliwaomba wananchi kuendelea kulipa kodi kwa maendeleo ya Jiji la Arusha na maendeleo yao, huku akiwataka watumishi kuendelea kukusanya mapato ya jiji hilo kwa uadilifu.

Kwa upande wake, Waziri Ummy alimshukuru Rais Samia kwa kufungua hospitali hiyo na kuahidi kuzitoa fedha hizo kabla ya Juni 30, mwaka huu kama alivyoagiza.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia Amuagiza Waziri Ummy Kutoa Bil. 1/= Ujenzi Hospitali Arusha
Rais Samia Amuagiza Waziri Ummy Kutoa Bil. 1/= Ujenzi Hospitali Arusha
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiOtIfTLg90WGW6-i5udq_7YAzWhmmfbjJZ7wdtCwpVP-J9jYFQNBp08T_tlYpUyGqlC_F2PsBSa-VVtxTTRlfnq6qD4pdQgqai3AEec0OjT-fgpitejoA31Y1Pl1XctBH5S6bZ67I7zvN-vxcD7P8-LPSONYL5S0dhITSsCwbrbe_cnI76rQ6lwf_inA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiOtIfTLg90WGW6-i5udq_7YAzWhmmfbjJZ7wdtCwpVP-J9jYFQNBp08T_tlYpUyGqlC_F2PsBSa-VVtxTTRlfnq6qD4pdQgqai3AEec0OjT-fgpitejoA31Y1Pl1XctBH5S6bZ67I7zvN-vxcD7P8-LPSONYL5S0dhITSsCwbrbe_cnI76rQ6lwf_inA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/rais-samia-amuagiza-waziri-ummy-kutoa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/rais-samia-amuagiza-waziri-ummy-kutoa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy