Mabalozi tangulizeni maslahi ya taifa - Waziri Mkuu
HomeHabari

Mabalozi tangulizeni maslahi ya taifa - Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabalozi wanaoteuliwa kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi wanapaswa kutanguliza maslahi ya Taifa katika...


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabalozi wanaoteuliwa kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi wanapaswa kutanguliza maslahi ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema kuwa mabalozi hao wanapaswa kutekeleza falsafa ya Mheshimiwa Rais Samia ya kuona kazi zilizoratibiwa zinaendelea kutekelezwa kwa uadilifu mkubwa na uaminifu ili ziweze kutoa matokeo chanya katika kila kazi zinazofanyika.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumapili, Oktoba 3, 2021) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma wakati alipokutana na mabalozi saba watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Sweden, Rwanda, India, Ethiopia, Uswisi na Jamhuri ya Korea.

Mabalozi hao na nchi zao kwenye mabano ni Luteni Jenerali Yacoub Mohamed (Uturuki), Grace Olotu (Sweden), Meja Jenerali Richard Makanzo (Rwanda), Anisa Mbega (India), Innocent Shiyo (Ethiopia), Hoyce Temu (Uswisi) na Togolani Mavura (Jamhuri ya Korea).

Waziri Mkuu amesema mabalozi hao wana jukumu la kukuza uchumi wa Tanzania kupitia diplomasia ya uchumi. “Waheshimiwa mabalozi mna jukumu kubwa la kukuza uchumi wetu. Nendeni mkaimarishe biashara na nchi yetu. Muangalie sisi tumefanya nini na tumepungua wapi na je tunaweza kurekebisha vipi,” amesema.

Amesema ili Tanzania iweze kupaa zaidi kiuchumi, inapaswa kukuza sekta ya viwanda hatua ambayo itafanya bidhaa zinazouzwa ziwe ni zile zilizosindikwa. “Mnalo jukumu la kuangalia ni namna gani tunaweza kuongeza uzalishaji na siyo wa mazao ghafi bali yaliyosindikwa. Tunataka tuuze kahawa iliyosindikwa hadi mwisho, na kama ni korosho, tuuze zilizobanguliwa.”

“Tanzania tunataka tuimarishe uchumi wetu wa viwanda. Kuna watu wanadai kuwa viwanda vingi vilivyokuwepo zamani vimekufa, lakini wanasahau kwamba teknolojia imebadilika sana. Kwa hiyo leteni watu kwenye uwekezaji wa viwanda, cha msingi wawe ni wale ambao wana historia nzuri kwenye nchi zao (genuine investors),” amesisitiza.

Amesema Tanzania imedhamiria kufufua mazao ya mkonge, michikichi na mbegumbegu za Mafuta na akawataka watafute wawekezaji makini ambao watakuja kuwekeza kwenye mazao hayo.

“Sambamba na hilo, muangalie uwezekano wa kupata masoko ya mazao yanayozalishwa nchini. Mnapaswa muwe ni kiungo baina ya nchi yetu na hizo nchi mnazoenda kutuwakilisha. Muangalie sisi tuna mazao au bidhaa gani na wao wanaweza kuagiza kiasi gani kutoka hapa nchini.”

Amewataka waangalie ni jinsi gani wanaweza kuinua sekta nyingine kama vile utalii kwa kuitangaza Tanzania huko waendako ili kuvutia watalii wengi zaidi. “Tanzania tuna fukwe nzuri sana kule Zanzibar na kuanzia Tanga hadi Mtwara. “Himizeni wawekezaji wa kujenga hoteli kwenye hizi fukwe ili watalii wakija wakute zile wanazozihitaji.”

Kuhusu wana-diaspora, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao wawatambue walioko huko waendako, watambue biashara na kazi zao na wawashawishi wafungue matawi ya kampuni zao huku kwao. Amewataka wasiache kuwapa taarifa za mara kwa mara juu ya mambo yanayofanyika hapa nchini.

“Pia angalieni fursa za masomo katika nchi mnazoenda ili Watanzania wapate fursa za mafunzo ya kitaalamu huko nje. Kumbukeni kuwa lugha yetu ya Kiswahili ina fursa nyingi za ajira kwa Watanzania, hivyo msiache kukitangaza Kiswahili katika nchi zenu,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka mabalozi hao waende wakaripoti mara moja kwenye vituo vyao vipya vya kazi. “Mmeshapata maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na hayo ndiyo maelekezo muhimu. Nendeni vituoni, muda umeisha. Huu siyo muda wa kwenda kuaga mawaziri. Wako wengi sana. Naamini baada ya kuonana na viongozi wetu wakuu, sasa mko imara.”

Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Luteni Jenerali Yacoub Mohamed alimshukuru Waziri Mkuu kwa nasaha alizowapa na kwamba zimewasaidia kutambua msimamo wa serikali ukoje.

“Tutajitahidi kutekeleza yote uliyotuelekeza kwa kadri ya uwezo wetu. Tunatambua uteuzi huu ni fursa kubwa na unaonesha imani aliyonayo Mheshimiwa Rais kwetu. Jambo kubwa tunaloondoka nalo, ni kuweka mbele maslahi ya Taifa letu,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mabalozi tangulizeni maslahi ya taifa - Waziri Mkuu
Mabalozi tangulizeni maslahi ya taifa - Waziri Mkuu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfCiQf0LIc_ixCVEShpl8CRTs-TYnhgJtljM034FuM8VnAGBwaxMI2hkWab3DUftr2rvE3-LGPFf-YCUKzXcceVlFYKXmUfQOWFe9hRUn8DSOMUjJKhkyKSZE3R05cSfiA9dYVIP9M_QD7/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfCiQf0LIc_ixCVEShpl8CRTs-TYnhgJtljM034FuM8VnAGBwaxMI2hkWab3DUftr2rvE3-LGPFf-YCUKzXcceVlFYKXmUfQOWFe9hRUn8DSOMUjJKhkyKSZE3R05cSfiA9dYVIP9M_QD7/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/mabalozi-tangulizeni-maslahi-ya-taifa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/mabalozi-tangulizeni-maslahi-ya-taifa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy