KOCHA wa zamani wa kikosi cha Arsenal, Arsene Wenger anaamini kwamba mchezaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland atakuja kucheza ndani ...
KOCHA wa zamani wa kikosi cha Arsenal, Arsene Wenger anaamini kwamba mchezaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland atakuja kucheza ndani ya Ligi Kuu England.
Katika usajili uliopita, Haaland alikuwa akihusishwa na timu za Ligi Kuu England ikiwa ni pamoja na Chelsea, Liverpool na Manchester United ila ngoma ikawa ngumu kukamilika.
Pia saini yake haikugombewa ndani ya Ligi Kuu England pekee hata Real Madrid, Barcelona zinazoshiriki La Liga nazo zilikuwa zinahitaji saini ya mshambuliaji huyo.
PSG pia inayoshiriki Ligue 1 nao walikuwa sokoni wakihitaji kupata saini ya mshambuliaji huyo anayetajwa kuwa moja ya washambuliaji bora kwa zama hizi za sasa.
Wenger amesema:"Nafikiri inaweza kutokea kucheza England kwani timu zake zinaonekana ziko vizuri kiuchumi kuliko zingine.
"Soka la England linatawala na lina fedha nyingi. Namuona Haaland atakuja kuwa mchezaji mkubwa na mwenye uwezo wa kufunga mabao mengi kama ilivyo kwa Mbappe, "Kylian),".
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS