WANAJESHI wa mpakani, Biashara United leo wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya FC Dikhil ya Dijibout utakaochezwa Stade du Ville. ...
WANAJESHI wa mpakani, Biashara United leo wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya FC Dikhil ya Dijibout utakaochezwa Stade du Ville.
Mchezo huo utachezwa leo Septemba 10, saa 9:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Katibu wa Biashara United, Haji Mtete amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo chanya.
"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya FC Dikhil na tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi tutafanya vizuri,".
Biashara United ya Mara ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS