BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba wamebainisha kuwa hawakustahili matokeo hay...
BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba wamebainisha kuwa hawakustahili matokeo hayo.
Kwa ujumbe huo ni kama wameyakataa matokeo hayo kwa kuwa walikuwa na nia ya kutwaa tena Ngao ya Jamii ila mambo yalikuwa magumu kwao ndani ya uwanja.
Bao pekee la Yanga lilipachikwa na Fiston Mayele kwa shuti kali lililomshinda Aishi Manula ambaye hakuwa na chaguo dakika ya 10 ya mchezo katika Uwanja wa Mkapa.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba, mabosi hao ambao walikuwa wanaitetea Ngao ya Jamii waliandika kwamba, "Hatukustahili matokeo haya,!"
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na ni kiashiria kwamba Ligi Kuu Bara inakwenda kuanza.
Kesho Septemba 27 ile burudani ya Ligi Kuu Bara inakwenda kuanza na mabingwa watetezi ni Simba.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS