HASSAN Mwakinyo, bondia Mtanzania amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Afrika, ABU katika pambano la uzito wa Super welterweight baada ya...
HASSAN Mwakinyo, bondia Mtanzania amefanikiwa kutetea
ubingwa wake wa Afrika, ABU katika pambano la uzito wa Super welterweight baada ya ushindi kwa TKO katika raundi ya nne.
Ilikuwa ni dhidi ya bondia Julius Idongo kutoka Namiba kwenye mchezo wa Mabingwa wa Ulingo uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza.
Ilikuwa ni katika pambano la raundi 12, Mwakinyo alishinda katika raundi ya nne na kumfanya aweze kutetea taji lake.
Baada ya ushindi huo Mwakinyo amesema kuwa ushindi huo ni kudra za Mungu na anashukuru kwa kushinda.
Kwa upande wa Mnamibia amesema kuwa haelewi imekuajekuaje akashindwa katika pambano hilo kwa kuwa anaamini katika uwezo wake.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS