MKUDE JONAS, MORRISON WAPIGWA BITI SIMBA NA GOMES
HomeMichezo

MKUDE JONAS, MORRISON WAPIGWA BITI SIMBA NA GOMES

  U NAAMBIWA!  Kocha Mkuu  wa Simba,  Didier Gomes  Da Rosa, amewataka  nyota wake wote waliopo  kwenye mapumziko  mafupi kutojisahau  kuf...


 UNAAMBIWA! Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, amewataka nyota wake wote waliopo kwenye mapumziko mafupi kutojisahau kufanya mazoezi binafsi wakiwemo Ousmane Sakho na Bernard Morrison, huku akisema atakayerejea mazoezini hana utimamu wa mwili atakiona cha moto.


Gomes alitoa mapumziko 
ya siku 10, kwa nyota wake baada ya kikosi hicho kurejea kutoka katika kambi yao ya maandalizi iliyokuwa nchini Morocco kwa wiki mbili.


Timu hiyo ipo mapumzikoni kupisha michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar.

 

Mmoja wa mabosi kutoka Benchi la Ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Gomes amewataka wachezaji wake ambao hawapo katika majukumu ya timu ya taifa, kuendelea kufanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kujiweka fiti.


Bosi huyo alisema kuwa hataki kuona mchezaji yeyote akiongezeka uzito mara baada ya timu itakaporejea kuendelea na mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya ‘pre-seasson’.


Aliongeza kuwa kocha huyo amepanga kuwapima uzito wachezaji wote kikosi hicho kitakaporejea kambini kuendelea na mazoezi.

 

“Kocha baada ya kuwapa mapumziko wachezaji ambao hawapo katika timu za taifa, haraka akaagiza kuwa kila mchezaji ahakikishe anafanya mazoezi ya kutosha ili mara atakaporejea kambini asije kuanza moja tena kutafuta utimamu wa mwili.

 

“Na hili alilikazia kwa Morrison, Mkude (Jonas) na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kuelekea msimu ujao.


“Kocha alisisitiza zaidi kwa hao kwa sababu anawajua wachezaji hao wana tabia za kula bata sana na mara kadhaa wanajikuta hata hawapati muda wa mazoezi nje ya timu, jambo ambalo kocha hataki kuona linatokea,” kilisema chanzo hicho.

 

Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kuwa:
“Benchi la Ufundi 
limepanga kukutana ndani ya siku hizi mbili kwa ajili ya kupanga siku ya kuanza na program za mazoezi.”



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MKUDE JONAS, MORRISON WAPIGWA BITI SIMBA NA GOMES
MKUDE JONAS, MORRISON WAPIGWA BITI SIMBA NA GOMES
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvEntDWrSK11I511PhfPn_NakGx62y8T_HIJeLVoGzJVYICEcQ9cqCY9HrLPYr4Gf7tKATS3UmqQlQQQN44lP5QB2DSfc27agpUyBMkiRT7C9dNCVkHLblvMLb_BWI99M45KQAGewA-szg/w640-h432/Mkude+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvEntDWrSK11I511PhfPn_NakGx62y8T_HIJeLVoGzJVYICEcQ9cqCY9HrLPYr4Gf7tKATS3UmqQlQQQN44lP5QB2DSfc27agpUyBMkiRT7C9dNCVkHLblvMLb_BWI99M45KQAGewA-szg/s72-w640-c-h432/Mkude+1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/mkude-jonas-morrison-wapigwa-biti-simba.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/mkude-jonas-morrison-wapigwa-biti-simba.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy