HILI HAPA JESHI KAMILI LA SIMBA 2021/22
HomeMichezo

HILI HAPA JESHI KAMILI LA SIMBA 2021/22

TAYARI kwa sasa mashabiki wa Simba wapo na shauku kubwa kuweza kuona namna gani watajitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia chama la...

KMC:TUTAYEYUSHA PIRA ICE CREAM LA AZAM FC
VIDEO:BREAKING: SERIKALI YAZUNGUMZIA KUHUSU SIMBA V YANGA
VIDEO: LIVE:KUHUSU KUYEYUKA KWA KARIAKOO DABI, SIMBA WATOA TAMKO, WAKILI AFUNGUKA

TAYARI kwa sasa mashabiki wa Simba wapo na shauku kubwa kuweza kuona namna gani watajitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia chama lao likitambulishwa pamoja na burudani za kutosha.


Ni leo Septemba 19, Uwanja wa Mkapa ambapo kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliliambia Spoti Xtra kuwa kila kitu kinakwenda katika mpangilio ni suala la mashabiki kuweza kununua tiketi kwa wingi na kujitokeza kushuhudia burudani na  timu itakayocheza mchezo wa kirafiki ambayo ni TP Mazembe ambayo ipo ndani ya Tanzania.


Hapa Spoti Xtra inakuletea chama kamili la Simba kwa msimu wa 2021/22 pamoja na wale warithi wa mikoba ya nyota ambao walisepa ndani ya kikosi hicho namna hii:-


Makipa


Aishi Manula na Beno Kakolanya hawa kwa upande wa makipa waliweza kuweka rekodi ya kuwa timu iliyoruhusu mabao machache ya kufungwa ambayo ni 14 katika mechi 34.


Manula ni kipa bora wa muda wote ndani ya Simba ambapo hata msimu uliopita wa 2019/20 alikusanya clean sheet 18.Msimu  wa 2020/21 alikusanya clean sheet 18 alicheza jumla ya mechi 26 kati ya 34 alitumia dk 2,278 huku Kakolanya alikaa langoni mechi 8. Kazi kubwa ni kuendeleza rekodi yao msimu ujao na Ally Salim alikwama kuanza langoni.


Mabeki



Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohamed Hussein,’Tshabalala’ Kenedd Juma, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Joash Onyango hawa wana kazi ya kuendelea pale ambapo waliishia. Kinara wa pasi za mwisho alikuwa ni Kapombe ambaye alitoa jumla ya pasi sita na alicheza mechi nyingi sawa na Tshabalala ambao kwa pamoja walicheza mechi 31.


Ukuta bora kwa msimu uliopita ulikuwa ndani ya Simba kwa kuwa waliruhusu mabao 14 katika mechi 34.


Viungo


Jonas Mkude, Rarry Bwalya, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu na Taddeo.  Lwanga hapa kesi kubwa iliyokuwa inatibulia viungo ni ile ya utovu wa nidhamu hasa kwa Mkude ambaye aliweza kusimamishwa mara mbili. Kwa kuwa ni familia hapa wanakazi ya kurekebisha doa hilo. Pia mzee wa kukera Morrison alikuwa na matukio yake kadhaa ambayo yalikuwa yakitafsiriwa kuwa ni utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kugombana na wachezaji uwanjani ikumbukwe ile mechi ya Simba 0-1 Ruvu Shooting.


Washambuliaji


Utatu ambao ulikuwa kwenye moto na kuweza kutupia jumla ya mabao 44 ni Meddie Kagere alitupia mabao 13,Chris Mugalu mabao 15 na kinara wao alikuwa ni nahodha Jonh Bocco mabao 16 kati ya 78 ambayo yalifungwa na timu hiyo wana kazi ya kuendelea pale walipoishia.


Wabeba mikoba



Katika maingizo mapya ya Simba kuna wawili ambao wanatajwa kupewa mikoba ya nyota wawili waliosepa ndani ya timu hiyo wakiwa wameacha alama kubwa msimu uliopita.


Ni Clatous Chama na mshikaji wake Luis Miquissone ambao walikuwa ni mhimili wa timu hiyo kwa upande wa viungo kutokana na kazi ambayo walifanya.


Kiungo Peter Banda anatajwa kuwa mrithi wa Luis. Ana kazi kubwa ya kuweza kufanya  makubwa ila haitakuwa kazi rahisi kwake kwa kuwa itahitaji muda kuweza kuwa kwenye ubora.Ikumbukwe kwamba Luis kwa msimu uliopita katika ligi aliweza kuwa namba mbili kwa watengeneza pasi za mwisho ambapo alitoa pasi 10 na kufunga mabao 9.


Sakho anatajwa kuwa mrithi wa Chama naye pia ana kazi ya kufanya kwa ajili ya kuweza kutimiza majukumu yake. Ikumbukwe kuwa Chama alikuwa ni kiungo bora wa muda wote ndani ya Simba. Msimu wa 2019/20 alikuwa ni kiungo bora alipofunga mabao mawili na pasi 10 na msimu wa 2020/21 Chama alifunga mabao 8 na pasi 13 hivyo sio kazi nyepesi kwa mrithi wa Chama kufanya kazi kama ya mwamba huyo wa Lusaka.


Hawa wanasubiriwa kutambulishwa


Jeremiah Kisubi huyu ni kipa inaelezwa kuwa ameshamalizana na Simba ni suala la muda tu kutambulishwa sawa na Kibu Denis.


Hawa hapa uhakika


Waliotambulishwa rasmi ni Peter Banda alikuwa anakipiga Big Bullet ya Malawi.Yusuph Mhilu msimu uliopita alikuwa Kagera Sugar.


 Duncan Nyoni alikuwa mali ya Klabu ya Silver Strike. Pape Ousmane Sakho alikuwa mali ya Tenghueth ya Senegal.



Henock Inoga Baka raia wa Congo, Israel Mwenda alikuwa ndani ya KMC msimu uliopita, Abdul Samad alikuwa Kagera Sugar, Emmanuel Mwanuke alikipiga Gwambina FC ya Mwanza na Sadio Kanoute, raia huyu wa Mali.


 



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: HILI HAPA JESHI KAMILI LA SIMBA 2021/22
HILI HAPA JESHI KAMILI LA SIMBA 2021/22
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbcrktYENW6EHsjWGLbp47zxZ3gsG8B_ZAl8MQUNRUFv72hN7ryUFJjVHK2vaKcJ4zD9J9FxB_olpZwM0DibPiPbPMmOYZrc4DEQaD1nTjjwCZlTF7JjRQCn895Z23P7wmzWePQToDEkmt/w640-h426/28_manula-196183927_551891942464633_891353540212491085_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbcrktYENW6EHsjWGLbp47zxZ3gsG8B_ZAl8MQUNRUFv72hN7ryUFJjVHK2vaKcJ4zD9J9FxB_olpZwM0DibPiPbPMmOYZrc4DEQaD1nTjjwCZlTF7JjRQCn895Z23P7wmzWePQToDEkmt/s72-w640-c-h426/28_manula-196183927_551891942464633_891353540212491085_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/hili-hapa-jeshi-kamili-la-simba-202122.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/hili-hapa-jeshi-kamili-la-simba-202122.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy