HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hajawahi kuwa Simba zaidi yeye alikuwa Yanga katika maisha yake yote. Kwa sasa Manara ...
HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hajawahi kuwa Simba zaidi yeye alikuwa Yanga katika maisha yake yote.
Kwa sasa Manara ni Ofisa Habari wa Yanga ambapo aliibuka huko muda mfupi baada ya kubwaga manyanga ndani ya Klabu ya Simba na huko alikuwa ni Ofisa Habari alidumu kwa muda wa miaka 6.
Manara amesema:"Nazungumzia fact, mimi sijawahi kuwa Simba na mimi sio Simba zaidi mimi ni Yanga.
"Moja ya kazi kubwa niliyoifanya labda ni kuonesha ukubwa feki hiyo dhambi niliitendea vibaya sana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nipo tayari kuhukumiwa hata gerezani kwa kufanya ulaghai wa kufix ukubwa ambao haupo.
Haji ameongeza kuwa Yanga ndio klabu yenye mataji mengi zaidi vinginevyo ni uongo ambao yeye mwenyewe hapo nyuma alishiriki kuupika.
Chanzo: E FM
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS