Dkt. Mwigulu Awakaribisha Wawekezaji Kutoka Misri
HomeHabari

Dkt. Mwigulu Awakaribisha Wawekezaji Kutoka Misri

Na. Josephine Majula, WFM, Cairo- Misri Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewakaribisha Wawekezaji kutoka Jamhuri ya...

Na. Josephine Majula, WFM, Cairo- Misri

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewakaribisha Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuwekeza na kufanya biashara na Tanzania kutokana na uwepo wa mazingira rafiki na fursa za uwekezaji.

 

Waziri nchemba ametoa rai hiyo mjini Cairo Misri, wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt International Cooperation Forum) lililowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo washirika wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Ulaya, Jumuiya ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia.

 

Dkt. Mwigulu alisema kuwa kuna umuhimu wa kusisitiza kukuza mahusiano ya kimataifa hususan kwa nchi za kiafrika zinazoendelea na kuweka mikakati endelevu ya kupambana na athari za janga la Uviko – 19, ili kukuza uchumi. 

 

“Katika Kongamano hili tumejadilia namna bora ya kusaidiana katika mitaji hususan katika nchi zenye Taasisi za Kifedha zenye uwezo wakutoa fedha katika mazingira ya Uviko- 19 kutokana kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi”, alieleza Dkt. Nchemba.

 

Aidha Dkt. Nchemba ameipongeza Wizara ya Ushirikiano ya Kimataifa ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa kuandaa kongamano hilo kwa kuwa limeunganisha wadau kutoka sehemu mbalimbali duniani na kutoa fursa ya kuweza  kujadiliana na kupeana uzoefu kwa lengo la  kuleta maendeleo.

 

Vilevile ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya uchumi, uwekezaji na biashara ili kukuza uchumi kati ya nchi hizo.

 

Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt International Cooperation Forum) linalofanyika kwa siku 2 limehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Malawi, Senegal, Kenya, Namibia na Zambia.

 

MWISHO.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Mwigulu Awakaribisha Wawekezaji Kutoka Misri
Dkt. Mwigulu Awakaribisha Wawekezaji Kutoka Misri
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFTF_LhmSTnNstXR01uuUsuQ87aELIk0aS2t_L7-gvlDTJ8UJvo31WkQTSw5CWvhRUIdLc9r5hUzucBK-AbSzeQX7OaF-G-mYKAoHPbk39eOR-J9u9rDu0nfmQyJnGIqrNuK_mZ0mYDT2J/s0/11.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFTF_LhmSTnNstXR01uuUsuQ87aELIk0aS2t_L7-gvlDTJ8UJvo31WkQTSw5CWvhRUIdLc9r5hUzucBK-AbSzeQX7OaF-G-mYKAoHPbk39eOR-J9u9rDu0nfmQyJnGIqrNuK_mZ0mYDT2J/s72-c/11.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/dkt-mwigulu-awakaribisha-wawekezaji.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/dkt-mwigulu-awakaribisha-wawekezaji.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy