Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Dkt.ndumbaro Aagiza Watumishi Wote Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kupitia Mafunzo Ya Kijeshi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wote wanaofanya kazi katika Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya ...


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wote wanaofanya kazi katika Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wajiandae kisaikolojia kupitia mfumo wa mafunzo ya Kijeshi.

Ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki  wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo Jijini Arusha ikiwa ni ziara ya kikazi Chuoni hapo ya kuwatembelea na kuzungumza na Watumishi hao ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi

Amesema mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia kwenda katika mfumo wa Jeshi Usu, yanalenga kuleta suluhisho la kudumu katika kukabiliana na changamoto za usimamizi wa rasilimali misitu na nyuki pamoja na wanyamapori  nchini.

Amesema hakuna Mtumishi yeyote wa Taasisi hizo  atakayekwepa mafunzo hayo kwa vile hiyo ni sera ya Wizara huku akisisitiza kuwa hilo halikwepeki na yeyote ambaye hayupo tayari basi ahame wizara hiyo ndiyo itakuwa salimika yake

" Leo unaweza kuhamishwa kutoka Olmotonyi kwenda Shirika la Hifadhi za Taifa ( TANAPA) au TFS wenzako kule washakamilika tayari ni  wanajeshi, wewe utakuwa raia" alihoji Dkt.Ndumbaro

Amesisitiza kuwa  kila mtumishi aliyeko katika Taasisi hizo lazima apitie mafunzo hayo kwa sababu watakuwa wakihamishwa kutoka Taasisi moja hadi nyingine ndani ya Wizara hivyo endapo hajapitia mafunzo hayo itamuwia vigumu katika kutekeleza majukumu yao wakati akiwa raia katika mfumo wa kijeshi.

Amezitaja Taasisi hizo kuwa ni Mfuko wa Misitu Tanzania (TFF)  Mfuko wa Wanyamapori Tanzania ( TWPF) Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) Chuo cha Taifa cha Utalii ( NCT) Chuo cha Misitu Olmotonyi, Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi,  Makumbusho ya Taifa (NMT), ChUo cha Nyuki Tabora (BTI),  Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Taasisi ya Utafirti wa Misitu (TAFORI) TAWA, TANAPA na TFS

Kupitia agizo hilo,Dkt.Ndumbaro amezitaka Taasisi hizo kujiandaa kushiriki katika mafunzo hayo ambapo amesema  mafunzo hayo yatatolewa  kwa awamu awamu.

Akizungumza na Watumishi hao wa Chuo cha Olmotonyi, Dkt.Ndumbaro amesema anataka wanavyowafundisha wanafunzi wao ambao wataajiriwa TFS inayoendeshwa kijeshi ni lazima wakufunzi wao wawe wanajeshi kwanza

" Haiwezekani mnawafundisha  Wanafunzi waende kuajiriwa huko TFS kama wanajeshi wakati ninyi sio wanajeshi, mnawafundisha nini  " alihoji Ndumbaro

Awali, Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof.Dos Santos Silayo alieleza kuwa kwa vile TFS ndo imekuwa muajiri mkuu wa Wahitimu wa Chuo hicho hivyo wameanza utaratibu wa kuhakikisha baadhi ya kozi katika Chuo hicho ziwe na mafunzo ya kijeshi ili kuwaandaa wanafunzi wa Chuo hicho wanapoajiriwa na TFS

Alisema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa wao kama TFS imekichagua Chuo hicho kuwa mojawapo ya kituo cha Mafunzo ya kijeshi kwa baadhi ya Maafisa kutoka TFS.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3479,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,618,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Dkt.ndumbaro Aagiza Watumishi Wote Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kupitia Mafunzo Ya Kijeshi
Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Dkt.ndumbaro Aagiza Watumishi Wote Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kupitia Mafunzo Ya Kijeshi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEht5TDSEHFqmYkm-JY9dPXR5BbbT9D73YQPDFbQWs6wnpsiqLqTY0x8C3c01XSqAQjIByG9xJw7l88W88eXgMf_cIN8rRN_MzV6kleGmnpMQhvMv4hdy4k6l5GJzGE3DvUUqVyk0gWzbOBE/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEht5TDSEHFqmYkm-JY9dPXR5BbbT9D73YQPDFbQWs6wnpsiqLqTY0x8C3c01XSqAQjIByG9xJw7l88W88eXgMf_cIN8rRN_MzV6kleGmnpMQhvMv4hdy4k6l5GJzGE3DvUUqVyk0gWzbOBE/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/waziri-wa-maliasili-na-utalii.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/waziri-wa-maliasili-na-utalii.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy