Waziri Ummy Ataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kushirikiana Na Makatibu Tawala Wasaidizi Mikoa
HomeHabari

Waziri Ummy Ataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kushirikiana Na Makatibu Tawala Wasaidizi Mikoa

  Na Angela Msimbira, NJOMBE Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu ameanza ziara ya kik...

TAMISEMI yatoa maagizo kwa mikoa kuhusu mikopo asilimia 10
Serikali Kuajiri Askari 600 Kukabiliana Na Wanyama Wakali Na Waharibifu
Majaliwa Aahidi Serikali Kutekeleza Maagizo Yaliyotolewa Na Katibu Wa Itikadi Na Uenezi CCM


 Na Angela Msimbira, NJOMBE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu ameanza ziara ya kikazi leo mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine atakagua miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya ngazi ya msingi, sekta ya elimu na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Akizungumza  Agosti 10,2021 na Sekretarieti ya Mkoa huo, Waziri Ummy ameupongeza uongozi na watendaji kwa kuendelea kwa kasi, ari na jitihada katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo na kuongoza kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka 2021/2022.

Amesema Sekretarieti za Mikoa zina wajibu wa kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa wananchi wanahitaji kupatiwa maendeleo na maendeleo yanapatikana kwa Halmashauri imara.

Katika ziara hiyo, Waziri Ummy amesisitiza umuhimu wa viongozi wa sekretarieti za Mikoa nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani kwa kuwa ndio wasimamizi wakuu katika ngazi ya Halmashauri.

Aidha, amesema kuwa Makatibu Tawala wasaidizi wa Mikoa wana wajibu wa kuhakikisha wanachambua bajeti za halmashauri na kuangalia vipaumbele ambavyo vinasaidia katika kutatua kero za wananchi zikiwemo ununuzi wa madawati, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali za Wilaya na ujenzi wa miundombinu ya Barabara.

“Makatibu Tawala wasaidizi wa Mkoa wanawajibu wa kuhoji na kuchambua bajeti za Halmashauri kwa kina, kwa kuangala vipaumbele vitakavyosaidia kutatua kero za hasa katika masuala ya elimu, afya na miundombinu kwa ujumla. Ni kazi yenu kufanya kazi hiyo na sio ofisi ya Rais TAMISEMI, Ni wajibu wenu kusimamia matumizi ya Halmashauri kwa kuhakikisha fedha zinapelekwa katika kutatua kero za wananchi,”amesisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotatua kero za wananchi.

Kabla ya kikao na Sekretarieti ya Mkoa, Waziri Ummy amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya na kukutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM).


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Ummy Ataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kushirikiana Na Makatibu Tawala Wasaidizi Mikoa
Waziri Ummy Ataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kushirikiana Na Makatibu Tawala Wasaidizi Mikoa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdImTAXhW6hP8KqrSqC-tEm-_5TYBqwVhyQgZikIth7Sb2g1K1Ovr29-wMIphAP0QXm_KHDwb9Jtnfiyv7CUZVY5T50Ehm5wdiQDisa1w9D-DS2gdUjii0kKLdSHW3tpb3qBeJUJZiUTJd/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdImTAXhW6hP8KqrSqC-tEm-_5TYBqwVhyQgZikIth7Sb2g1K1Ovr29-wMIphAP0QXm_KHDwb9Jtnfiyv7CUZVY5T50Ehm5wdiQDisa1w9D-DS2gdUjii0kKLdSHW3tpb3qBeJUJZiUTJd/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/waziri-ummy-ataka-wakurugenzi-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/waziri-ummy-ataka-wakurugenzi-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy