UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kila kitu kuhusu kambi na maandalizi ya msimu wa 2021/22 yanakwenda sawa. Kaimu Ofisa Habari wa Si...
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kila kitu kuhusu kambi na maandalizi ya msimu wa 2021/22 yanakwenda sawa.
Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu mpango kazi wa timu hiyo.
"Mzigo wa jezi upo na tutautambulisha wiki moja kabla ya siku ya Simba day. Mambo yanakwenda vizuri na kuanzia msimu ujao tutafanya kwa uzuri zaidi.
"Kuhusu kambi ya Simba iliyopo Morocco huko kila kitu kinakwenda sawa kuanzia kwa wachezaji wenyewe wanasema kuwa kambi ni nzuri," .
Simba inayonolewa na Gomes imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.
Septemba 25 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba v Yanga utakaokuwa ni wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Septemba 29.
Kambi ya Simba imejumuisha wachezaji wapya ikiwa ni pamoja na Duncan Nyoni, Abdul Samad, Peter Banda.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS