Ole Sabaya Aanza Kujitetea Mahakamani
HomeHabari

Ole Sabaya Aanza Kujitetea Mahakamani

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi kwa kutumia silaha aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabay...


Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi kwa kutumia silaha aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya ameanza kutoa utetezi wake  jana  katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha .


Akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi Odira Amworo akiongozwa na wakili  wake Moses Mauna mstakiwa huyo Lengai Ole Sabaya ameielezea mahakama kuwa  mnamo tarehe tisa mwezi wa pili 2021  alikuwa Bomang'ombe makao makuu ya wilaya ya Hai  na alikuwa  anaongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya  kuanzia asubuhi saa tatu na nusu hadi saa nane na nusu mchana.  

Sabaya amesema kuwa baada ya kumaliza kikao hicho saa nane mchana hadi saa tisa kasoro alipokea maelekezo na mamlaka za uteuzi ikamtaarifu kuwa kuna watu wameshuka Uwanja wa Ndege wa KIA na alipaswa  kuwachukua na kuambatana nao kwaa ajili ya kuwafikisha mkoani  Arusha.

Ndipo baada ya hapo aliwatafutia gari huku akiwa na gari lake binafsi ambalo alikuwa anaendeshwa na dereva wake huku jumla wakawa na magari mawili nakuanza safari kwenda Arusha huku aliokuwa amewachukua walikuwa na taarifa walichoagizwa huko Arusha.

Amesema mahakamani kuwa ilipofika saa saa kumi na moja na dakika arobaini na tano jioni walifika Arusha  baada ya kufika walienda eneo ambalo walielekezwa kwa ajili ya kufanya mahojiano na muhusika  ambae ni mmliki wa duka la shahidi Store Muhamed Saad  lakini hakumkuta.

amesema baada ya kumkosa mmiliki huyo licha ya watu hao waliongozana nao ambao hakuwataja mahakamani hapo na kudai hawahusiki na shitaka hilo walikuwa na taarifa zote kwamba watamkuta mmiliki huyo.

Sabaya amesema kuwa  baada ya kumkosa mmiliki huyo alifanya mawasiliano na mamlaka waliopewa maelekezo hayo kisha ikawaambia kuwa wameshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha hivyo hao watu waliowakuta katika duka hilo wapelekwe kituo cha polisi kwa sababa watasaidia kupatikana kwa muhusika na yeye akaelekezwa kuwasiliana nae huyo mkuu wa wilaya.

Akaeielezea mahakama kuwa mshtakiwa wa pili Silvesta Nyegu hakuwepo katika tukio hilo na mshtakiwa wa tatu Daniele Mbura hamfahamu kabisa na wala hajawahi kuonana nae maisha yake yote .

Amesema kuwa Bakari Msangi hakupigwa kama anavyodai na alichokielezea mahakamani hapo ni uongo na yeye hamfahamu kama amepigwa na kwamba Bakari Msangi ameamua kufanya hivyo kutokana na ugomvi wa kisiasa wa muda mrefu baina yake na yeye baada ya  kumshinda katika uchaguzi wa kiti uwenyekiti wa umoja wa wavijana chama cha mapinduzi yeye pamoja na wenzake.

Hakimu mkazi Mwandamizi Odira Amworo ameahirisha kesi mpaka Jumatatu tarehe 16 Agosti 2021 ambapo mshatakiwa huyo ataendelea kutoa utetezi wake.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ole Sabaya Aanza Kujitetea Mahakamani
Ole Sabaya Aanza Kujitetea Mahakamani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCp8h8SP2cdxEpgo8suu9lK91qDQH_iavcJwtB462O9AsTxrnVWfr9e_8W5_7DbKqtKpvIgoINeg4YlfKB7dCh62VPpDAUunH98pYffRiuAj_UTaNp4e4jMxBLELAJk917hXUPWKjmG9wW/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCp8h8SP2cdxEpgo8suu9lK91qDQH_iavcJwtB462O9AsTxrnVWfr9e_8W5_7DbKqtKpvIgoINeg4YlfKB7dCh62VPpDAUunH98pYffRiuAj_UTaNp4e4jMxBLELAJk917hXUPWKjmG9wW/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/ole-sabaya-aanza-kujitetea-mahakamani.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/ole-sabaya-aanza-kujitetea-mahakamani.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy