Majaliwa: Tutaienzi Mipango Iliyoachwa Na Kwandikwa
HomeHabari

Majaliwa: Tutaienzi Mipango Iliyoachwa Na Kwandikwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali na itatekeleza mipango yote iliyoachwa na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Tai...

Jeshi la Polisi linachunguza kifo cha Padri.
Serikali Kuendelea Kuboresha Makazi Bora Kwa Wahudumu Wa Afya.
Spika Dkt. Tulia Ampongeza Rais Samia Kuzindua Royal Tour


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali na itatekeleza mipango yote iliyoachwa na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, marehemu Elias Kwandikwa.

Amesema kuwa Serikali itaenzi mipango yake na itahakikisha ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni katika Jimbo la Ushetu zinatekelezwa kama alivyoahidi.

Amesema hayo  Jumatatu (Agosti 9, 2021) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya marehemu Kwandikwa kijijini kwao Butibu, Ushetu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania, wana-Shinyanga na wana-Ushetu waenzi mambo yote mazuri yaliyoachwa marehemu Kwandikwa.

“Tumepoteza kiongozi aliyekuwa anaongoza majeshi yetu, amefanya kazi nzuri sana katika kipindi chote cha uhai wake alipokuwa anaitumikia Serikali; marehemu alikuwa mwadilifu, muwajibikaji na aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa.”

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wabunge, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa George Simbachawene amesema marehemu Kwandikwa alikuwa ni kiongozi ambaye alitekeleza majukumu yake sawasawa na alihakikisha matokeo yanaonekana.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Faraji Mnyepe amesema marehemu Waziri Kwandikwa ameondoka wakati wizara ikiwa inamuhitaji kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka. “Marehemu Waziri Kwandikwa alikuwa ni kiongozi mwenye upendo wa hali ya juu na alikuwa mtenda haki kwa kila mtu.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amesema marehemu Waziri Kwandikwa alikuwa ni mtu wa kipekee, msikivu na mnyenyekevu.

Amesema kuwa marehemu Waziri Kwandikwa, alikuwa ni mwepesi wa kujifunza mambo ya kijeshi na alilisaidia jeshi kwa kadri ya uwezo wake katika kipindi chote alichokuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

“Alikuwa ni kiongozi asiyependa kukaa muda mwingi ofisini bali aliwatembelea makamanda maafisa katika maeneo yao ya kazi ili kuona utendaji kazi na changamoto zinazowakabili.”

Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo amesema marehemu Waziri Kwandikwa ameacha pengo kwani katika kipindi chote amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Serikali, CCM na wananchi wa ushetu na Watanzania kwa ujumla.

“Tumepoteza kiongozi hodari, mahiri na CCM tumepoteza mtu aliyekipenda chama kwa moyo mkuu. Mwenyezi Mungu aendelee kuwa mfariji kwa familia, wana-Ushetu, wana-Shinyanga na Watanzania kwa ujumla.”

Awali, Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi na Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki Kahama, Askofu Ludovick Joseph Minde amesema marehemu Waziri Kwandikwa alikuwa ni mnyenyekevu, mwenye busara, hekima na mpenda maendeleo.

Aidha, Askofu Minde aliongeza kuwa marehemu Kwandikwa alikuwa mfadhili mkubwa katika maendeleo ya kiroho na kimwili.

Marehemu Waziri Elias Kwandikwa alizaliwa Julai 7, 1966 wilayani Kahama, Shinyanga na alifariki Agosti 2, 2021 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Majaliwa: Tutaienzi Mipango Iliyoachwa Na Kwandikwa
Majaliwa: Tutaienzi Mipango Iliyoachwa Na Kwandikwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwnixbCKQXrcMpN_UdBBe4LdEuq28zUVBcA1rCtxObr3_qE1n__YhhKa2wi_vQqzl6yFWewUZBQWdwg7KJR9fqKJEbXoOCxBa-gR_2m-QFSNCY5fkjYWPcWRs-60MslZeaftN9o3TqVFEg/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwnixbCKQXrcMpN_UdBBe4LdEuq28zUVBcA1rCtxObr3_qE1n__YhhKa2wi_vQqzl6yFWewUZBQWdwg7KJR9fqKJEbXoOCxBa-gR_2m-QFSNCY5fkjYWPcWRs-60MslZeaftN9o3TqVFEg/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/majaliwa-tutaienzi-mipango-iliyoachwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/majaliwa-tutaienzi-mipango-iliyoachwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy