Maafisa Ustawi Watakiwa Kuwajibika Kusaidia Watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu amewaagiza maafisa ustawi wa jamii kutimiza majukumu yao kwa...

 


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu amewaagiza maafisa ustawi wa jamii kutimiza majukumu yao kwa kufuata kanuni zilizowekwa ili kuepusha madhara mbalimbali yanayotokana na ukiukwaji wa sheria.

Akizungumza na Maafisa Ustawi pamoja na wadau mbalimbali mjini Morogoro, Dkt. Jingu amesema baadhi ya madhara ya kutotimiza wajibu ni pamoja na watoto kufanyiwa ukatili katika jamii zinazowazunguka.

“Kifungu namba 158 cha Katiba ya nchi yetu kinazungumzia juu ya wajibu wa  wanajamii na watu wanaomiliki sehemu za starehe  kutokuruhusu utoaji wa burudani kwa watoto nyakati za usiku. Bado wanajamii wanawatumia watoto kwenye  utoaji wa burudani nyakati za usiku na hata wazazi kuwatuma watoto wao kwenye sehemu hizo kununua vitu kama sigara na Vilevi.” alisema Dkt Jingu.

Aliongeza kuwa Serikali pamoja na wadau wa masuala ya ustawi wa jamii imeona kuna haja wa kuweka kanuni na sheria zinazohusu maadili katika lugha rasmi na rahisi kwani kanuni zipo lakini pengine wanajamii hawazielewi.

Aliendelea kwa kusema kwamba kumekuwa na wimbi la watu mbalimbali wanaodhalilisha watoto kwa kutokufuata kanuni zilizowekwa.

“Baadhi ya wadau wanafanya baadhi ya mambo kwa nia nzuri lakini wanajikuta wanakosea. siku hizi kuna tabia ya kuwadhalilisha watoto waliofanyiwa ukatili kama kubakwa kwa kuwaweka kwenye mitandao bila kujali  kuwa kile kitu kitakuwa na madhara ya kudumu kwa mtoto yule maana kuweka kitu kwenye mtandao ni kuipa nafasi dunia nzima kuona”

Dkt John Jingu alimalizia kwa kusema kuwa urahisishaji wa lugha inayotumika kwenye  kanuni na sheria unaweza ukasaidia kupunguza  makosa yanayojitokeza kwa wanajamii kushindwa kuzitasfiri vyema kanuni hizo.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Maafisa Ustawi Watakiwa Kuwajibika Kusaidia Watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi
Maafisa Ustawi Watakiwa Kuwajibika Kusaidia Watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIvPTQqmdXxlBSeWWo9fPYetgkUo32VDP83Ke7AQjVhJ8X0xm3g7-Ixr5fu3xU4q2xABnclV2dCikqIvRa2LvE2eB2n4NPnqf1HQ5m4lqNhDU2TNeELuIoBe_QlXhxS6V9WS1FOjmAmU39/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIvPTQqmdXxlBSeWWo9fPYetgkUo32VDP83Ke7AQjVhJ8X0xm3g7-Ixr5fu3xU4q2xABnclV2dCikqIvRa2LvE2eB2n4NPnqf1HQ5m4lqNhDU2TNeELuIoBe_QlXhxS6V9WS1FOjmAmU39/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/maafisa-ustawi-watakiwa-kuwajibika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/maafisa-ustawi-watakiwa-kuwajibika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy