UONGOZI wa Yanga umemtambulisha nyota mpya leo Agosti 10,2021 ambaye ni kipa kutoka Aigel Noir. Ni Erick Johola ambaye ni raia wa Tanzan...
UONGOZI wa Yanga umemtambulisha nyota mpya leo Agosti 10,2021 ambaye ni kipa kutoka Aigel Noir.
Ni Erick Johola ambaye ni raia wa Tanzania na alionekana na Yanga katika siku ya Mwananchi.
Nyota huyo anakuwa ni kipa namba mbili baada ya kipa namba moja Diarra Djigui kutambulishwa ndani ya kikosi hicho na ni dili la miaka miwili ambalo amesaini.
Anakuja kuchukua nafasi ya Farouk Shikalo ambaye dili lake limeisha sawa na Metacha Mnata ambapo makipa hawa wote wawili hawajaongezewa kandarasi mpya.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS