Naibu Waziri Mabula Aibukia Kanisani Na Kuhimiza Ulipaji Kodi Ya Ardhi
HomeHabari

Naibu Waziri Mabula Aibukia Kanisani Na Kuhimiza Ulipaji Kodi Ya Ardhi

Na Munir Shemweta, SONGWE Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameibuka katika Kanisa Katoliki Paroki...


Na Munir Shemweta, SONGWE
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameibuka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwambani katika kata ya Mkwajuni wilayani Songwe na kuwahimiza waumini wa kanisa hilo kuhakikisha wanalipa kodi ya pango la ardhi.

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo jana akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi kwenye mkoa wa Songwe Dkt Mabula alisema, wamiliki wote wa ardhi nchini wanapaswa kulipa kodi ya pango la ardhi ili kuongeza mapato na kuiwezesha Serikali   kuwatumikia wananchi katika shughuli za maendeleo.

Aliwaeleza waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwambani kuwa, ardhi ni mali na mtaji na katika kuitunza lazima iongezwe thamani kwa kupangwa, kupimwa na kumilikishwa

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, ardhi inaweza kutumiwa na wamiliki wake katika shughuli za maendeleo sambamba na  kupunguza migogoro ya ardhi hasa ile ya mipaka na kusisitiza kuwa mmiliki anapaswa kuwa na hati ili kuwa na usalama wa miliki yake.

‘’ukiwa na ardhi iliyopimwa utapunguza migogoro ya mipaka na majirani zako, usikae na ardhi bila kuipima, watu wanaongezeka kila siku ila ardhi haiongezeki na ninyi mmejaliwa kuwa na madini na kama una ardhi hakikisha una hati itakuja kukusaidia hapo baadaye’’. Alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema Wizara yake imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali inakwisha na kubainisha kuwa moja ya jitihada hizo ni uanzishwaji wa ofisi za ardhi za mikoa ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

 Naibu Waziri Mabula amemaliza ziara yake katika mkoa wa Songwe ambapo mbali na kusikiliza na kuitafutia ufumbuzi migogoro ya ardhi katika mkoa huo alizindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya katika mkoa wa Songwe,


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Naibu Waziri Mabula Aibukia Kanisani Na Kuhimiza Ulipaji Kodi Ya Ardhi
Naibu Waziri Mabula Aibukia Kanisani Na Kuhimiza Ulipaji Kodi Ya Ardhi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVslOu117zur8ZSN56Cpihg5igz9FaxLYjsV1EraPg9WdtRcrDN6kYW2lJNXK6Txu544HxbLHBDidLvkgfbF42ZV6xa94W6k5TskKv3eTHBTam8vWm9jvvFRn1FNqQG8b8OGuGbyV5Eow9/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVslOu117zur8ZSN56Cpihg5igz9FaxLYjsV1EraPg9WdtRcrDN6kYW2lJNXK6Txu544HxbLHBDidLvkgfbF42ZV6xa94W6k5TskKv3eTHBTam8vWm9jvvFRn1FNqQG8b8OGuGbyV5Eow9/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/naibu-waziri-mabula-aibukia-kanisani-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/naibu-waziri-mabula-aibukia-kanisani-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy