GSM YAKUBALI KUFANYA KAZI NA MANJI NDANI YA YANGA
HomeMichezo

GSM YAKUBALI KUFANYA KAZI NA MANJI NDANI YA YANGA

  W ADHAMINI  wa  Yanga Kampuni  ya GSM rasmi  imekubali kufanya  kazi pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu  hiyo, Yusuf Manji katika...

 


WADHAMINI wa Yanga Kampuni ya GSM rasmi imekubali kufanya kazi pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji katika kuelekea msimu ujao.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Manji ahudhurie katika mkutano mkuu wa klabu hiyo wa kupitisha katiba mpya ya mfumo wa mabadiliko uliofanyika Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa DYCCC, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

 

Muunganiko huo wa GSM na Manji huenda ukaongeza hamasa ya wachezaji na mashabiki katika kuelekea dabi ya Simba dhidi ya Yanga.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said, alisema kuwa mabadiliko ya Yanga siyo kwa ajili ya kumnufaisha mtu mmoja pekee, bali yapo kwa ajili ya kuinufaisha klabu.

Hersi alisema kuwa, wao GSM wapo tayari kushirikiana na kufanya kazi na Manji katika kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kuijenga Yanga itakayokuwa tishio na mfano wa kuigwa barani Afrika.

 

Aliongeza kuwa wanatambua mchango wa Manji katika kuijenga Yanga itakayokuwa imara na kikubwa kuhakikisha wanachukua mataji yote ya ubingwa watakayoshiriki katika msimu ujao.

 

“GSM hatupo hapa kwa ajili ya kujinufaisha sisi tupo kwa ajili ya kuijenga klabu yetu ya Yanga na kikubwa tunataka kuifanya kuwa mfano wa kuigwa kama zilivyo baadhi ya klabu kubwa Afrika ambazo zimepiga hatua za kimafanikio.

 

"Hivyo tunamkaribisha Manji muda wowote kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja na hatimaye tufanikishe malengo yetu ya pamoja, ninaamini uwepo wake utaifanya klabu kufikia mafanikio mazuri.

 

"Siyo Manji pekee, milango ipo wazi kwa watu au makampuni mengine yatakayotaka kuja kuisaidia klabu yetu ya Yanga, tunatakiwa kufanikisha malengo tuliyojiwekea kwani timu inatakiwa kuwa na wawekezaji zaidi ya mmoja,” alisema Hersi.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: GSM YAKUBALI KUFANYA KAZI NA MANJI NDANI YA YANGA
GSM YAKUBALI KUFANYA KAZI NA MANJI NDANI YA YANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyQ6Gm3Rk-Qxrd0sC1LkS_vU2_tSJoVOtMXhMEwo9_UhNKtI8RvhbL4cFSRxXI3mGT842ihqziUQ2adTDAENMy7sp42bpBilH_Iirhhka7u5F2FverSkg6yh-uwyEseNqegwf1UiLDlOK7/w640-h550/yangasc-208553364_4200211993391597_50219627741217331_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyQ6Gm3Rk-Qxrd0sC1LkS_vU2_tSJoVOtMXhMEwo9_UhNKtI8RvhbL4cFSRxXI3mGT842ihqziUQ2adTDAENMy7sp42bpBilH_Iirhhka7u5F2FverSkg6yh-uwyEseNqegwf1UiLDlOK7/s72-w640-c-h550/yangasc-208553364_4200211993391597_50219627741217331_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/gsm-yakubali-kufanya-kazi-na-manji.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/gsm-yakubali-kufanya-kazi-na-manji.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy