KIUNGO wa Azam FC, Salum Aboubakary, 'Sure Boy' anatajwa kuwa katika rada za mabosi wa Yanga huku wenye mali nao wakihitaji hu...
KIUNGO wa Azam FC, Salum Aboubakary, 'Sure Boy' anatajwa kuwa katika rada za mabosi wa Yanga huku wenye mali nao wakihitaji huduma yake.
Ikumbukwe kuwa msimu uliopita wa 2019/20, Yanga walikuwa na mpango wa kumsajili nyota huyo ambapo ishu ilikuwa katika dau.
Yanga wao waliweka dau la milioni 40 jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Azam FC wawaambie kwamba waongeze dau kwa kuwa Sure Boy ni nembo ya Azam FC jambo lililokwamisha dili hilo.
Kwa sasa mkataba wa nyota huyo ambaye yupo katika kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars unakaribia kumeguka jambo ambalo linawapa nguvu Yanga kuipata saini yake.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS