RASMI BEKI AS VITA ASAINI MIAKA MIWILI, AWAAGA WACHEZAJI WAKE
HomeMichezo

RASMI BEKI AS VITA ASAINI MIAKA MIWILI, AWAAGA WACHEZAJI WAKE

SASA ni rasmi Yanga imemsainisha beki wa kulia  wa AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo,  Shaaban Djuma kwa mkataba wa miaka miwili  kwa a...


SASA ni rasmi Yanga imemsainisha beki wa kulia wa AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo, Shaaban Djuma kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.


Djuma Shaaban unakuwa ni usajili wa kwanza wa Yanga wa kimataifa ambapo klabu hiyo imelenga kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo timu hiyo ina nafasi kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.


Yanga chini ya mwenyekiti msaidizi wa kamati ya usajili, Eng. Hersi Said, imesema kuwa timu hiyo itafanya usajili wa maana kwa ajili ya kufanya vizuri kwa msimu ujao katika mashindano yote ambayo watashiriki.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja Mkuu wa AS Vita, Yves Dida Ilunga, alikiri wazi kuwa Klabu ya Yanga tayari imekamilisha usajili wa beki huyo na hivi karibuni watatangaza dili hilo.


“Kila kitu kimekamilika, Yanga imeshakamilisha taratibu zote za kumsajili Djuma, nadhani hivi karibuni kila kitu kitakuwa wazi juu ya dili la beki huyu, tunasubiri taratibu tu za timu ila kila kitu kimemalizika,” alisema meneja huyo.


Kwa upande wa meneja wa mchezaji huyo, Faustino Mukandila, yeye alisema: “Yanga imefanikiwa kumsajili mteja wangu, Shaaban Djuma, hivyo itoshe watu wafahamu kuwa kila kitu kimekamilika siku siyo nyingi tutangaza dili hilo kuwa lipo tayari.”


Naye nahodha wa Klabu ya AS Vita na timu ya taifa ya Congo, Jeremy Mumbere, alifunguka juu ya dili la nahodha mwenzake wa klabu hiyo Shaaban Djuma kujiunga na Yanga.

“Tayari Djuma amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga, mimi tayari ameniaga kuwa atajiunga na Yanga mara baada ya kumalizika kwa mchezo wetu wa mwisho wa ligi tutakaocheza Juni 6 (Jumapili).


“Ameniambia kuwa amesaini mkataba na Yanga wa miaka miwili, hivyo baada ya mchezo wa mwisho ataanza mipango ya safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wake,” alisema nahodha huyo wa AS Vita.

Naye Djuma mwenyewe tulipomtafuta kuzungumza kuhusu usajili wake wa kujiunga na Yanga, alisema: “Nafikiri taratibu zilizobaki ni kwa upande wa Klabu ya Yanga na AS Vita kuweka wazi dili hili, nachofahamu kila kitu kimekamilika, nasubiri wao waweke wazi ishu hii ili kila mtu afahamu kinachoendelea.”

Tulipomtafuta Makamu Mwenyekiti Kamati ya Usajili ndani ya Yanga, Eng.Hersi Saidi kuzungumzia juu ya usajili wa beki huyo simu zake ziliita bila majibu.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: RASMI BEKI AS VITA ASAINI MIAKA MIWILI, AWAAGA WACHEZAJI WAKE
RASMI BEKI AS VITA ASAINI MIAKA MIWILI, AWAAGA WACHEZAJI WAKE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjP-RjOn12F7iqEPw0G8xpIx2u7WWJC0XHBIQOVpLqjMnv6ZxrYnmlWW2J0Ggjl7MvaxkVzSprhFF0ID2Pv0iaiAIi1MjYbNZXndR_jOif7k8b6OojVlf8q8w1UYGOl6eFcwoLRXsVogXON/w516-h640/Djuma.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjP-RjOn12F7iqEPw0G8xpIx2u7WWJC0XHBIQOVpLqjMnv6ZxrYnmlWW2J0Ggjl7MvaxkVzSprhFF0ID2Pv0iaiAIi1MjYbNZXndR_jOif7k8b6OojVlf8q8w1UYGOl6eFcwoLRXsVogXON/s72-w516-c-h640/Djuma.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/rasmi-beki-as-vita-asaini-miaka-miwili.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/rasmi-beki-as-vita-asaini-miaka-miwili.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy