MANYAMA KUONGEZA VITA YA NAMBA NDANI YA SIMBA
HomeMichezo

MANYAMA KUONGEZA VITA YA NAMBA NDANI YA SIMBA

  IMEELEZWA kuwa ikiwa usajili wa nyota wa kikosi cha Ruvu Shooting Edward Manyama ukikamilika basi itakuwa ni vita mpya ya namba ndani y...

 


IMEELEZWA kuwa ikiwa usajili wa nyota wa kikosi cha Ruvu Shooting Edward Manyama ukikamilika basi itakuwa ni vita mpya ya namba ndani ya kikosi hicho.

Imekuwa ikielezwa kuwa Manyama ambaye ni beki wa kushoto wa Ruvu Shooting ambaye pia aliwahi kucheza timu ya Namungo FC yupo kwenye rada za Simba.

Tetesi hizo zimekwenda mbali na kubainisha kwamba tayari nyota huyo amesaini dili la miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.


Kwa sasa nafasi hiyo ndani ya Simba yupo nahodha msaidizi Mohamed Hussein ambaye yupo pia kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, mshindani wake ni Gadiel Michael na wakati mwingine Erasto Nyoni naye amekuwa akipewa jukumu hilo.

 Gadiel  ambaye yeye alijiunga na Simba akitokea Yanga naye amekuwa akipata changamoto kubwa kutoka kwa Mohamed ambaye ameongeza dili la miaka miwili hivi karibuni.

Ikiwa Manyama atajiunga na Simba basi kazi kubwa itakuwa kwenye utatu huo unaonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kuweza kupambania namba kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ruvu Shooting zimeeleza kuwa beki huyo mkataba wake upo ukingoni hivyo anaweza kujiunga na timu yoyote ambayo itaweka dau nono. 

Manyama alikuwa kwenye rada za Yanga msimu uliopita ambapo dili lake baada ya kubuma akaibukia ndani ya Ruvu Shooting akitokea ndani ya Namungo FC.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MANYAMA KUONGEZA VITA YA NAMBA NDANI YA SIMBA
MANYAMA KUONGEZA VITA YA NAMBA NDANI YA SIMBA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGglBfCe3C_0UEnEIlWV5O1BsjarSP2x7oFX6DdNPDiUwX2k-HnE1pa5Lg2lmwWdXhiVcx_vKcKyhzj0xe_OWgH37-1s4fpHOTjzPiHm2bvBCMts5Qf_6HknapYZphaN8ETKHjXZanVUdz/w640-h640/official_mohamedhussein15-195267758_494603691775768_7721183263621493676_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGglBfCe3C_0UEnEIlWV5O1BsjarSP2x7oFX6DdNPDiUwX2k-HnE1pa5Lg2lmwWdXhiVcx_vKcKyhzj0xe_OWgH37-1s4fpHOTjzPiHm2bvBCMts5Qf_6HknapYZphaN8ETKHjXZanVUdz/s72-w640-c-h640/official_mohamedhussein15-195267758_494603691775768_7721183263621493676_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/manyama-kuongeza-vita-ya-namba-ndani-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/manyama-kuongeza-vita-ya-namba-ndani-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy