NYOTA wa kikosi cha Al Hilal, kiungo Last Jesi inaelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Azam FC kwa dili la miaka miwili. Nyota huyo inael...
NYOTA wa kikosi cha Al Hilal, kiungo Last Jesi inaelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Azam FC kwa dili la miaka miwili.
Nyota huyo inaelezwa kuwa alikuwa anapigiwa hesabu na Simba ambayo ilimuona katika mashindano ya Simba Super Cup 2021.
Taarifa kutoka mtu wa karibu wa nyota huyo imeeleza kwamba tayari ameshaanza mazoezi ndani ya Uwanja wa Azam Complex.
"Jesi ameanza mazoezi ndani ya Uwanja wa Azam Complex hivyo kama Simba ama Yanga wanamhitaji itakuwa mpaka Azam FC wenyewe waamue kumuacha," ilieleza taarifa hiyo.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS